Waziri wa Nishati Mhe Medard
Kalemani akizungumza na Waandishi wa habari hawapo picha,alipofanya
ziara ya kukagua athari zilizotokana na mvua iliyosababisha kufunguliwa
kwa maji katika bwawa la kuzalishia umeme kidatu Wilayani kilombero,
kulia Ni Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Mussa Zungu aliyeambatana
naye kujionea athari hizo.
Waziri wa Muungano na Mazingira
Mhe Mussa Zungu akitoa maelekezo kwa timu ya watalaam wa Nemc waliofika
kujionea athari za mvua katika mto Ruaha Mkuu unaotenganisha Wilaya ya
kilombero na Kirosa Mkoani Morogoro.
*************************************
NaFarida Saidy,Morogoro.
Kufuatia athari zilizojitokeza za
mafuriko kwa baadhi ya vijiji vya wilaya ya kilombero mkoani Morogoro
baada ya maji kufunguliwa katika bwawa la kufua umeme la Kidatu mawaziri
wawili wa Nishati Dkt.Medard Kalemani na Mussa Zungu wa Muungano na
Mazingira wamefanya ziara ya kukagua madhara yaliyojitokeza katika
Wilaya hiyo.
Lengo la ziara hiyo ni kunagalia
namna ya kudhibiti uharibufu uliojitokeza katika mabwawa ya kuzalishia
umeme ya Mtera na Kidatu,ambapo Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani
amewataka wananchi wanaofanya shughuri za kibinaadamu pembezoni mwa mto
Ruaha mkuu kuacha mala moja kwani wanaharibu mazingira.
Hata hivyo Waziri kelemani
amesema wao Kama wizara ya Nishati wanawajibu wa kulinda na kutunza
miundombinu yote ya uzalishaji wa umeme, hivyo wanashirikiana na Nemc na
wadau wengine wa mazingira ili kuulinda mradi mkubwa wa bwawa la kufua
umeme la Julius NyerereMW 2115,kwani maji yanayotoka katika mto Ruaha
Mkuu ndioyanayoenda katika mradi huo mkubwa wa kufua umeme wa Julius
NyerereMW 2115.
Kwa upande wake Waziri wa Muungano
na Mazingira Mhe Mussa Zungu amewataka Nemc kwa kushirikiana na wadau
wote wanaohusika na Mazingira kukutana ndani ya sikuku kumi ili kutoa
tathmini ya uharibifu uliotokea katika kipindi ambacho maji
yamefunguliwa katika mabwawa ya Mtera na Kidatu.
Hata hivyo kwasasa maji yamepungua
katika mto Ruaha Mkuu ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo maji
hayo yalitishia hata uhai wa daraja la mto huo linalotenganisha wilaya
mbili za Kilosa na Kilombero
Aidha mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Loata Ole Sanare anabainisha namna ambavyo wananchi wake waliathirika
huku wengine wakikosa makazi ya kwa sababu ya maji kujaa kwenye maeneo
yao, huku mwenyekiti wa bodi ya baraza la taifa ya mazingira akibainisha
moja ya kisababishi cha athari zilizojitokeza Ni wananchi kufanya
shughuri za kibinaadamu ikiwemo Kilimo kwenye kingo za mto huo.
Kujaa kwa mabwawa ya kufua umeme hapa nchini ni kiashiria cha
No comments :
Post a Comment