Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha huko kwenye
kitongoji cha Oloshoo kata ya Enguserosambu Tarafa ya Loliondo wilayani
Ngorongoro wamefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK 47 yenye
namba H 49 ikiwa na risasi 12 iliyokuwa njiani kufanya uhalifu kwenye
Mbuga za wanyama.
Aidha kwa muktadha huo Mapambano dhidi ya
matukio ya uhalifu na wahalifu ambapo kwa kipindi hichi wahalifu wengi
hudhani jeshi la polisi limelala hivyo niwahakikishie hatujalala na
tunaendelea kufanya misako na opereseheni mbalimbali iwe wakati wa mvua
Jua Tope au Masika Baridi au kiangazi kuhakikisha wahalifu hawapati
nafasi ya kutenda uhalifu.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa
kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana alisema kuwa kikosi
hicho kabambe baada ya kupewa taarifa fiche kuwa kuna watu 4 wawili
watanzania na wakenya wawili wameonekana maeneo ya Mpakani wakiwa
wanajipanga kuwinda wanyama adimu kwenye mbuga zetu muhimu.
Kwa mujibu wa Kamanda Shana baada ya kupata
taarifa hizo kikosi kazi chenye askari machachari wazalendo na wenye
weledi wa hali ya juu waliendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini juu
ya taarifa hiyo na tarehe 10.6.2020 tulifanya msako mkali katika kijiji
hicho kuwatafu wahalifu hao.
Alisema kuwa katika msako huo wahalifu wawili
walikamatwa wakiwa na silaha moja ya kivita aina ya AK 47na risasi zake
12 ndani ya magazine ambao majina yao tunayahifadhi kwa ajili ya
uchunguzi huku jeshi hilo likiendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili
waliokimbia nchi jirani ya Kenya.
Aidha jeshi la polisi linawasaka wahalifu hao
kujisalimisha mara moja kituo chochote cha polisi kwani wasipofanya
hivyo tutalazimika kutumia nguvu kubwa kuwatafuta ili hatua kali za
kisheria zichukuliwe.
Kamanda Shana akatumia fursa hiyo kuendelea
kuwashukuru wananchi ambao wameendelea kutoa taarifa mbalimbali za
uhalifu na wahalifu huku akiwataka kuendelea kushirikiana na vyombo vya
ulinzi na usalama katika kuwafichua wale wote wenye nia ovu ili kumaliza
uhalifu kwenye mkoa wetu.
Amebainisha kuwa Jeshi hilo mkoani hapa
linaahidi litatoa donge nono kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazo
fanikisha kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na Uwindaji haramu
,Ujambazi ,na uhalifu wa aina yeyote.
No comments :
Post a Comment