Mshindi wa wiki wa shindano la
TUSUA MAPENE NA VODACOM, Neema Laiser ( katikati) mfanyabiashara, mkazi
wa mtaa wa Uswahilini Jijini Arusha, akikabidhiwa mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi milioni 10 toka kwa Meneja mkakati wa Masoko
Vodacom kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama (kulia) na Meneja Mauzo
mwandamizi wa Vodacom kanda hiyo, Nathanael Pedigando
………………………………………………………………………………
Shindano la Tusua mapene na
Vodacom linaloendelea kote nchini, linawawezesha watumiaji wa mtandao
wa Vodacom kuweza kujishindia kitita cha milioni 10 kila wiki na wengine
waliobaki watajishindia zawadi ndogo ndogo. Hili ni shindano lilioanza
mwaka 2017, na kuendelea kuwanufaisha wateja wa Vodacom nchini.
Ili kushiriki kwenye promosheni
hii, mteja anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544,
kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Unaponunua tiketi, moja kwa moja
unaingia kwenye droo, washindi wa droo wanaingia kwenye Mpambano
ambapo wanatumiwa neno maalum ” keyword ” watakayoituma kwenda 15544
ili kuweza kukomboa zawadi. Wa kwanza kutuma neno hilo ataibuka na
kitita cha shilingi milioni 10, na wengine wanajipatia zawadi ndogo
ndogo.
Akikabidhi mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi milioni 10 za kitanzania, Meneja Mauzo mwandamizi wa
Vodacom kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama alimpongeza mshindi na
kuhamasisha wateja kushiriki Zaidi ili kuweza kujishindia zawadi kemkem.
Nae
mshindi wa zawadi ya Tusua mapene kutoka Arusha mjini, Mfanyabiashara
Neema Laiser aliwashukuru Vodacom kwa kuanzisha shindano hili ambalo
limemuwezesha kujishindia pesa itakayomuwezesha kuongeza mtaji na hivyo
kuimarisha biashara yake.
“Kwa
kweli sikuamini nilipopigiwa simu nikajua mambo ya uwongo, lakini kumbe
ni kweli na nawashauri watu wasiache kutumia mtandao wa Vodacom maana
ushindi kama huu unaweza kukukwamua kiuchumi” alisema Laiser.
No comments :
Post a Comment