Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame
Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).
Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara
ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imemtaja aliyeteuliwa kuwa ni Mhandisi
Tamimu Twaha Katakweba. Aidha, kufuatia uteuzi huu Mhandisi Katakweba
anakuwa Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MORUWASA.
Uteuzi huu umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019.
No comments :
Post a Comment