Muonekano wa Chelezo (kulia)
ambacho kimekamilika kwa asilimia mia moja na maendeleo ya Ujenzi wa
Meli Mpya ya MV Mwanza (kushoto) ambayo ujenzi wake umefikia zaidi ya
asilimia 30 katika bandari ya Mwanza South, Mkoani Mwanza
Mafundi wa Kampuni ya Gas Entec
kutoka Korea ya Kusini, wakiendelea na kazi ya ujenzi wa meli Mpya ya MV
Mwanza katika bandari ya Mwanza South. Meli hiyo inatarajiwa
kukamilika mapema mwaka 2021.
Mafundi wa Kampuni ya Kampuni ya
Songoro Marine Limited, wakikamilisha kazi ya upakaji rangi kwenye meli
ya MV. Butiama, katika bandari ya Mwanza South. Ukarabati wa meli
umefikia asilimia 99.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa maelekezo kwa Kaimu
Meneja wa Bandari ya Mwanza, Bw. Michael Palangyo,alipokagua maendeleo
ya ukarabati wa jengo la abiria katika bandari ya Mwanza North, mwishoni
mwa wiki.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akikagua maendeleo ya ukarabati
wa jengo la abiria katika bandari ya Mwanza North, mwishoni mwa wiki.
Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli. Bw. Eric Hamis.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto), akimsikiliza
Meneja Mradi wa meli mpya ya MV Mwanza, Mhandisi Vitus Mapunda, wakati
akimweleza namna ya ukataji wa vyuma wakati Naibu Waziri huyo alipokagua
maelekezo ya ujenzi wa meli hiyo, mwishoni mwa wiki.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………………………………………………………………………
Serikali imesema Meli ya MV
Butiama, MV Viktoria na Chelezo zitakabidhiwa wakati wowote kuanzia
sasa
baada ya ukarabati mkubwa uliofanyika kukamlika kwa asilimia mia moja.
Akizungumza mara baada ya
kukagua maendeleo ya ujenzi Meli mpya ya MV Mwanza Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kufunguliwa
kwa anga la Tanzania kutaruhusu wataalam kutoka nje kuwasili na kufanya
ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kutumia meli hizo na chelezo.
“Tungekuwa tushaanza kuzitumia
meli hizi kwani ukarabati wake umekamilika kwa asilimia 99, ni imani
yangu kuwa wataalam wanaosubiriwa watawasili siku chache zijazo na
kukamilisha kile kilichobaki ili wananchi waanze kutumia usafiri huu’
amesisitiza Naibu Waziri Mhandisi Nditiye
Naibu Mhandisi Nditiye amesema
pamoja na miradi hiyo Mradi wa Meli mpya ya MV Mwanza ujenzi wake
unaendelea kwa kasi na unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2021.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamis ameishukuru Serikali kwa
kukamilisha malipo yote Mradi wa Ukarabati wa meli hizo pamoja na
chelezo na kuahidi kuendelea kuisimamia kwa karibu ujenzi wa meli mpya
unaoendelea.
Naye Meneja Mradi wa Meli mpya
ya MV Mwanza, Mhandisi Vitus Mapunda amesema mradi wa meli hiyo
unaendelea vizuri na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kukamilisha tabaka
la chini la meli hiyo kabla ya kuiweka kwenye chelezo.
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri Mhandisi Nditiye amekagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la
abiria katika bandari ya Mwanza North na kutoa wiki moja na nusu
ukarabati huo kukamilika.
Kaimu Meneja wa Bandari ya
Mwanza, Michael Palangyo amemthibitishia Naibu Waziri Mhandisi Nditiye
kuwa mradi huo wa ukarabati utakamilika kwa wakati na viwango ili kuweza
kutoa huduma bora wakati meli za MV Butiama na Mv Viktoria zitakapoanza
kutoa huduma kwa wakati wa Mwanza, mikoa ya jirani na visiwa
vinavyozunguka mkoa huo.
No comments :
Post a Comment