Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe Constantine Kanyasu akizungumza katika mkutano
uliowakutanisha kwa pamoja Wadau wa Uhifadhi kujadili jinsi ya kulinda
shoroba ya Kwakuchinja pamoja na maeneo mengine muhimu ya Wanyamapori
katika ikolojia ya Tarangire na Manyara katika mkutano uliofanyika
katika wilaya ya Babati mkoani Manyara. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Babati, Mhe.Elizabeth Kitundu na kushoto ni Mkurugenzi wa Wanyamapori,
Dkt.Maurus Msuha.
Mkurugenzi wa Sheria
wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy Saleko akitoa ufafanuzi wa
kisheria kuhusu utekelezaji wa mkakati wa kulinda shoroba na maeneo
mengine muhimu ya Wanyamapori katika Ikolojia ya Tarangire na Manyara
katika mkutano uliofanyika katika wilaya ya Babati.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya
Burunge iliyopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Mkurugenzi wa Utafiti
wa TAWIRI, Dkt.Julius Keyyu akichangia hoja katika mkutano wa Wadau wa
Uhifadhi uliolenga kujadili jinsi ya kulinda shoroba na maeneo mengine
muhimu katika ikolojia ya Tarangire na Manyara.
Baadhi ya Wadau wa Uhifadhi walioshiriki katika mkutano huo uliofanyika katika wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa
Maliasili na IUtalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisisitiza jambo katika
mkutano wa wadau wa Uhifadhi wa kijadili namna ya kulinda shoroba
uliofanyika katika wilaya ya Babati mkoani Manyara.
…………………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ametoa agizo kwa Shirika
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuongeza idadi ya mabango ya barabarani
yanayoonyesha tahadhari na faini kwa madereva watakaogonga wanyamapori
katika barabara ya Babati kuelekea Arusha.
Ametoa agizo hilo
katika wilaya ya Babati mkoani Manyara katika mkutano wa Wadau wa
Uhifadhi uliowakutanisha Wataalamu mbalimbali kujadili namna ya kulinda
mapito asili ya wanyamapori (shoroba) pamoja na maeneo mengine muhimu
ya wanyamapori ambayo yapo hatarini kutoweka kufuatia kushamiri kwa
shughuli za kibinadamu
Mhe.Kanyasu amesema
kukosekana kwa tahadhari hizo kunatishia kuharibika kwa ikolojia ya
Tarangire na Manyara kutokana na idadi kubwa ya wanyamapori kuuawa kwa
kugongwa na magari kila siku.
Kwa mujibu wa
takwimu jumla ya wanyamapori 588 wakiwemo simba na twiga waliuawa mwaka
jana kwa kugongwa na magari yanayopita kwa spidi katika barabara hiyo
Kufuatia hali hiyo,
Mhe.Kanyasu ameitaka TANAPA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanyamapori
ya Burunge kukutana na Uongozi waTANROAD ili waweze kutekeleza agizo
hilo la uongezaji mabango katika barabara hiyo.
Akizungumzia mazimio
ya Mkutano huo, Mhe. Kanyasu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii kuunda kikosi kazi cha wataalamu mbalimbali kwa
ushirikiano wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Babati kutambua mipaka ya
shoroba katika vijiji
Mbali na maazimio hayo, Mhe, Kanyasu amemtaka
Mkuu wa wilaya ya Babati Kuhakikisha maeneo ambayo tayari yanatambulika
kuwa ni shoroba yalindwe ili yasiendelee kuvamiwa.
Aidha, Mhe.Kanyasu
amemtaka Mkuu wa wilaya ya Babati kuhakikisha anatoa maagizo kwa
Uongozi wa vijiji vinavyozunguka shoroba hawagawi maeneo ambayo ni
shoroba kwa Wananchi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu ikiwemo
ujenzi na kilimo.
Mbali na kuweka
mabango Mhe.Kanyasu amesema kuna haja ya kuweka kamera barabarani ili
kupunguza vifo vya wanyamapori wanaouawa kwa kugongwa na magari
yanayopita mwendokasi katika barabara ya Babati kuelekea Arusha.
Akitaja athari za
kuziba shoroba hizo,Mhe.Kanyasu amesema hali hiyo ikiendelea hivyo
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire itakuwa kisiwa na hivyo kuwafanya
wanyamapori wakiwemo tembo ambao husafiri kwenda kuzaliana na ukoo
mwingine wataanza kuzaliana ndugu kwa ndugu na hivyo kusababisha athari
kubwa kijenetiki.
Kwa upande Mkuu wa
wilaya hiyo, Elizabeth Kitundu amesema wananchi waliopo katika maeneo ya
Shoroba wamekuwa wakitambua umuhimu wa maeneo hayo na wamekuwa wakitoa
ushirikiano kwetu
Kutokanana hali hiyo,
” Ninakuahidi kupitia maafisa Ustawi wa Jamii tutendelea kutoa elimu
kwa wanavijiji wanaoendesha shughuli za kibinadamu katika maeneo ya
shoroba wafahamu kuwa ni hatari kwao na hivyo maeneo hayo yaachwe kwa
ajili ya wanyamapori huku mchakato wa kisheria ukiendelea kutekelezwa.
No comments :
Post a Comment