Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyeketi katikati) akimsikiliza Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF , Zuhura Mdungi aliyesimama akitoa neno la kuwakaribisha Wandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ofisi ndogo taasisi hiyo jijini Dar es salaam. Kulia kwa kwake ni Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF
,Ladislaus Mwamanga amekutana na Wandishi wa Habari jijini Dar es salaam
na kuwajulisha kuwa mipango ya kuanza utekelezaji wa kipindi cha pili
ambayo imezingatia maelekezo ya Serikali inaelekea kukamilika.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF
amesema katika kutekeleza kipindi hicho cha pili, Mfuko huo utajikita
zaidi katika kuhamasisha Walengwa kutumia zaidi huduma za kielektroniki
hususani katika suala la ulipwaji wa ruzuku.
Aidha Mwamanga amesema mkazo
mkubwa utawekwa katika kuhamasisha Walengwa kushiriki kwenye miradi ya
maendeleo hususani katika sekta za elimu,afya maji na shughuli za miradi
ya kiuchumi kwa kutumia utaratibu wa Ajira ya Muda na kisha kulipwa kwa
mujibu wa taratibu zilizopo.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF
ametoa wito maalum kwa Walengwa wa Mfuko huo kuhakikisha kuwa wanapata
huduma za simu ili waweze kunufaika na utaratibu mpya wa kulipwa kwa
njia ya kielektroniki ambao umefanyiwa majaribio kwenye halmashauri za
wilaya zipatazo 16 kwa mafanikio.
Bwana Mwamanga amezitaja
halmashauri ambazo Walengwa wa TASAF hulipwa kwa njia ya kieleketroniki
kuwa ni pamoja na Arusha, Ilala,Temeke, Kinondoni,Mpanda na Kigoma
Manispaa. Nyingine ni Bagamoyo,Songea Manispaa,Kisarawe, Kilwa, Muheza
,Mkuranga, Bahi,Urambo, Siha na Unguja.
Mfuko wa Maendeleo yas Jamii-TASAF
unatekeleza kipindi cha pili cha awamu ya tatu ambacho kilizinduliwa na
Rais John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam ambacho kinatarajiwa
kutumia kiasi cha shilingi trilioni 2.032 ambazo zitatumika kutekeleza
miradi inayolenga kuboresha huduma za miundombinu kwenye sekta za
afya,elimu na maji na kutoa ruzuku kwa kaya zinazoishi katika mazingira
duni sana ili ziweze kuboresha maisha.
No comments :
Post a Comment