Mkuu wa mkoa Kagera Bri.Gen Marco Gaguti aliyeshika ufunguo wenye kamba nyekundu akikabidhi boti kwa watendaji wa kata.
Mkuu wa mkoa Kagera anawahuitubia
wavuvi pamoja na wananchi katika kijiji cha katembe Kata Nyakabango
wilayani Muleba wakati wa hafla ya kukabithi Boti.
Wananchi pamoja na viongozi wa wilaya Muleba wakimsikiliza Mkuu wa mkoa alipokuwa akiwahutubia.
……………………………………………………………………………………..
Na Allawi Kaboyo,Muleba
Kufatia kuwepo
kwa vitendo vya uvuvi Haramu katika ziwa Victoria,Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amekabidhi boti tatu mpya kwa
watendaji wa
Kata za Bumbire na Ikuza na boti moja kubwa kwa sekta ya
uvuvi kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu wilayani Muleba.
Zoezi hilo
lilifanyika katika kijiji cha Katembe Kata Nyakabango wilayani Muleba
ambapo mkuu huyo aliipongeza halmashaurihiyo kwa jitihada kubwa
inazozifanya katika kuhakikisha serikali inaendelea kupata mapato hasa
kupitia uvuvi na kuzitaka halmashauri nyingine kuiga mfano huo.
“Naipongeza
sana Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa utekelezaji mzuri wa shughuli
za maendeleo hususani ukusanyaji wa mapato ya ndani ambapo kwa miaka 3
mfululizo imeongoza kwa ukusanyaji mapato uliovuka malengo ya mwaka kwa
mkoa wa Kagera, na hapa nitoe malekezo mahususi kwa harmashauri nyingine
kuiga mfano huu.” alieleza Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.
Gaguti
amewataka watendaji waliokabithiwa boti hizo kuhakikisha wanazifanyia
kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi maana hakuna
tena visingizio vya kwenda kuwahudumia wananchi kwa kigezo cha usafiri,
na kuwasihi kutozitumia kama fimbo ya kuwanyanyasa wananchi badala ya
kuwahudumia.
Aidha,
amewasihi wananchi kuanza kujishughulisha na uvuvi wa kisasa kwa kuwa na
vikundi vitakavyowawezesha kupata fedha kutoka taasisi za kifedha Pia
watumie zana za kisasa na kuwa malengo ya kufanya uvuvi wa kibiashara
hata kwa nje ya nchi na kueleza kuwa mkoa umejipanga kuleta wawekezaji
watakaowekeza katika sekta ya uvuvi.
“Tunatakiwa
kujua kuwa Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kimkakati kwa maendeleo ya nchi,
sisi kama Serikali ya mkoa tunao mpango wa kuwaleta wawekezaji watakao
wekeza katika sekta ya uvuvi hivyo ni wasihi wananchi na wavuvi tufanye
uvuvi wa tija wenye kufata taratibu zote kwa kutumia nyezo
zinazoruhusiwa, tutakuwa waajabu kama tutawaleta wawekezaji na tukakutwa
sisi wazawa ndo sababu ya kubwa ya kuendeleza uvuvi haramu katika ziwa
letu.” Alisisitiza Gaguti.
Akisoma
taarifa kwa mkuu wa mkoa, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
Bw.Emanuel Shelembi alisema kuwa upatikanaji wa boti hizo utasaidia
ufanisi katika utendaji kwenye visiwa hivyo ikiwemo kuthibiti uvuvi
haramu, kuthibiti utoroshwaji wa mazao ya samaki, kusaidia ufatiliaji wa
mapato pamoja na kurahisisha usafiri kwa watumishi waishio visiwani.
“Upatikanaji
wa boti hizi tatu unafanya kuwa na jumla ya boti nne zilizonunuliwa
katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John
Pombe Magufuli ikiwemo boti iliyonunuliwa katika kipindi cha 2018/2019,
hata hivyo boti hizi unazozikabithi zote zimenunuliwa zikiwa na vifaa
vyote vya usalama na uokoaji kama vili life jacket 38 na maboya matatu
kwa kila boti ambavyo vitatumika wakati wote chombo kitakapokuwa
majini.” Alisema Shelembi
Kwaupande wao
watendaji waliokabithiwa boti hizo wameishukuru serikali kwa kuwajali na
kuwapatia usafiri na kueleza kuwa wamekuwa wakitaabika hasa nyakati za
usiku kufanya doria na kazi mbalimbali katika visiwa hivyo suala
lililokuwa likipelekea kuhatarisha maisha yao nap engine doria
kutofanikiwa kutokana na kutumia boti za wavuvi.
Boti hizo
zimenunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani ambapo boti kubwa imegharimu
Tsh. 103,887,534.00 na boti mbili ndogo kila moja imegharimu Tsh.
34,789,780.00 na zote zimekabithiwa kwa wahusika ambapo Boti kubwa ina
injini mbili zenye nguvu ya (Horse Power) HP 85 kila injini moja ina
uwezo wa kubeba watu 16-18. Na boti mbili ndogo zenye injini moja moja
kila injini ina nguvu ya (Horse Power) HP 40 kila moja ina uwezo wa
kubeba watu 8-12.
No comments :
Post a Comment