Mwandishi wa habari masanja mabula
akifanya mahojiano na asha rajab mkaazi wa kiwani wilaya ya mkoani
aliyepewa talaka na mume wake baada ya kupata ulemavu wa miguu akiwa
ndani ya ndoa, kwa sasa asha anaishi na watoto wake watatu.
Mwandishi wa
habari masanja mabula akizungumza na mzee Haji Jeilan Aleyi (71) ambaye
ni baba mlezi wa asha rajab huko kiwani wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini
Pemba.
Picha na Masanja Mabula.
…………………………………………………………..
Na Masanja Mabula ,Pemba.
CHAMA cha wandishi
wa habari wanawake Tanzania –TAMWA-Ofisi ya Pemba kimepenga kumwezesha
kwa kumpatia elimu ya ujasiriamali Asha Rajab Shaban mjane na mlemavu wa
miguu anayeishi Kijiji cha Mbayayani Shehia ya Kiwani Mkoa wa Kusini
Pemba .
Mratibu wa TAMWA
Pemba Fat-hiya Mussa Said alisema mchakato wa kupeleka wataalamu wa
elimu ya ujasiriamali unaendelea ili kumwezesha kupata kazi
itakayomwingizia kipato.
“Sisi TAMWA
tumeguswa na hali hiyo , ambapo kwa sasa tunaendelea na mchakato wa
kumpelekea walimu watakao mpatia elimu ya ujasiriamali wa kutengeneza
sabuni na kusuka”alisema.
“Ukiachilia mbali
ulemavu pia anawatoto watatu na ukiangalia hana kazi inayompatia kipato ,
hivyo akipatiwa elimu ya ujasiriamali itamsaidia yeye na familia
yake”aliongeza.
Kauli hiyo ya
TAMWA imekuja baada Asha Rajab Shaban 26 ambaye ni mlevu wa miguu
kuomba kupatiwa elimu ya ujsiriamali ili aweze kuendesha maisha yake.
Asha alipata
ulemavu huo akiwa ndani ya ndoa hali iliyosababisha kupewa talaka na
aliyekuwa mume wake alisema elimu hiyo itamwezesha kujitegemea na
kuondokana na hali ya utegemezi aliyonayo kwa sasa.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Mbayayani, Kiwani alisema
zipo shughuli za ujasiriamali anaweze kuzifanya ikiwemo kutengeneza
sabuni, kusuka makawa pamoja na kushona.
“Nikiwa elimu ya
ujasiriamali nitaweza kuendesha maisha yangu na kuondokana na utegemezi
katika maisha yangu pamoja na familia yangu”alisema.
Mratibu wa
wanawake na watoto wa shehia ya Kiwani Mwanaidi Vuale Khatib alisema
vikao vya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo vimefanyika bila mafanikio.
Alisema kwamba
lengo ni kufanyika vikao ilikuwa ni kumtaka aliyekuwa mume wake aendelea
kutoa huduma kwa watoto ikiwemo nguo, chakula pamoja na kusimamia
watoto waende skuli.
Kwa upande wake
baba mlezi wa mjane huyo Haji Jeilan Aleyi (71) aliomba wahisani
kumsaidia kwani anapata shida kutokana na kukosa kazi ya kumuingizia
kipato.
“Hapa nategemea
kilimo kupata mahitaji ya familia yangu, naomba kama kunamwenye uwezo
kusaidia mahitaji ya chakula , makazi na nguo za watoto”aliomba.
Ustadhi Salum
Mohammed Haji alisema kwa mujibu wa dini ya Kiislamu ni kosa kumwacha
mwanamke aliyepata ulemavu akiwa ndani ya ndoa.
Sheha wa shehia ya
Kiwani Abdalla Makame Hamad alikiri kuwepo na tukio na kuahidi kuchukua
kila jitihada kumweezesha kupata haki yake za msingi.
No comments :
Post a Comment