……………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -PEMBA.
MZEE Haroub Ali
Kombo miaka 75 mkazi wa kisiwa cha Fundo Mkoa wa Kaskazini Pemba
amefikishwa ofisini kwa mkuu wa mkoa huo baada ya kushitakiwa na mzee
mwenzake
mwenye umri sawa (jina linahifadhiwa) akimlalamikia kwamba
anamchukulia mke wake.
Hii ni mara ya
pili wazee hao kufikishana mbele ya serikali ya Mkoa kutafuta ufumbuzi
wa tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu sasa.
Akitoa maelezo
yake , malalamikaji(jina tunalo)alisema mzee mwenzake ameshindwa
kuheshimu makubaliano ya awali na bado anaendelea na tabia yake.
Alieleza kwamba pamoja na makubaliano ya awali yaliyofanyika mbele ya uongozi wa Mkoa, ameshindwa kuyatekeleza naumia sana.
“Inauma sana kuona
mke wangu anachukuliwa na mzee mwenzangu , naomba Mhe Mkuu wa Mkoa
unisaidia ili tuikomesha tabia hii”alisema.
Katika maelezo
yake , Haroub Ali Kombo alisema amechoshwa na maneno hayo na kwamba
anajiandaa kuhama kisiwani humo na kurudi kwao Kiwani Mkoa wa Kusini
Pemba.
“Kwa kuwa
limenitokea mimi naonekana mkorofi, hivyo mhe Mkuu wa Mkoa namuomba
sheha aende kusimamia kuuza mazao yangu ili nirudi nilikotoka
Kiwani”alieleza.
Alisema tangu
walipoitwa kwa mara ya kwanza yeye alikata mawasiliano na mwanamke huyo
hata vipndo walivyokuwa wakilima pamoja waligawana.
Sheha wa shehia ya
Fundo Khamis Abeid alikiri kuendelea mawasiliano kati ya mzee huyo na
mwanemke huyo licha ya hapo awali wawili hao kutakiwa kukatisha
mahusiano.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Wete Kepteni Khatib Khamis Mwadini alitaka sheria zaa
kinidhamu zichukuliwe kwa mze huyo kwani ameshindwa kuheshimu maamuzi
yake mwenyewe.
“Kikao kilichopita
mzee huyu aliahidi kwamba anaenda kuhamisha mali zake ili arudi
alikotoka , lakini kumbe alikuwa anafanya utani , lazima alazishw
kushehimu maamuzi yake”alisema.
Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman alisema serikali haiwezi kuchezewa
hivyo mzee huyo anapaswa kuchukuliwa hatua kali.
Alisema awali mzee
Haroub kwa kinywa chake alitamka kuvunja mahusiano na mke wa mtu na
kutaka mashamba na vipando walivyolima pamoja vigawanywe ili kila mmoja
ili mawasiliano yasiwepo.
“Mwenye mke
analalamika kwamba bado unaendelea na mahusiano na mke wake, hivyo
serikali inachokihofia na kutokea ambayo hayakutarajiwa”alisema.
Hata hivyo kwa
mara nyengine Mzee Haroub aliomba serikali isimchukulie hatua kali kwani
, alimtaka Sheha wa shehia hiyo kumtafutia wateja kwa ajili ya kuuza
mazao yake .
No comments :
Post a Comment