Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani( pili kulia) aliyeambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
TANESCO, akipita kukagua shughuli za ujenzi wa upanuzi wa kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, Aprili, 30,2020,
katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani(,( mwenye kofia nyeupe) akiwa na Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi ya
TANESCO) akimueleza jambo Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dkt, Alexander
Kiyarunzi (kushoto) walipotembelea eneo la kuhifadhi nguzo wakati wa
ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na kufua umeme
cha Zuzu jijini Dodoma, Aprili 30,2020.
Vijana wakiendelea na kazi ya
ujenzi katika kituo cha kupoza na kusambaza na umeme cha Zuzu jijini
Dodoma, wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO ya kukagua ujenzi wa upanuzi
wa kituo hicho Aprili 30,2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (katikati) pamoja na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO
wakipata maelezo kutoka kwa msimamizi mkuu wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, baada ya kufanya ziara ya
kukagua ujenzi wa upanuzi wa kituo hicho, Aprili 30,2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani( katikati) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya
TANESCO wakati wa kikao baada ya ziara ya kukukagua ujenzi wa upanuzi wa
kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, Aprili
30,2020, kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani( katikati) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
TANESCO wakati wa kikao baada ya ziara ya kukukagua ujenzi wa upanuzi wa
kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, Aprili
30,2020, kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
TANESCO wakimsilikiza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( hayupo
pichani) wakati wa kikao baada ya ziara ya kukukagua ujenzi wa upanuzi
wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma,Aprili
30,2020.
…………………………………………………………………………………………………
Na Zuena Msuya Dodoma,
Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme nchini( TANESCO) kuendelea kukata
umeme kwa wadaiwa sugu ili kukusanya mapato zaidi na kulipa madeni ya
shirika hilo.
shirika hilo.
Dkt. Kalemani alisema hayo, Aprili
30, 2020, Jijini Dodoma, alipokutana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
wa TANESCO, kuzungumzia tathimini ya miaka mitano ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali, baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi
wa kutuo cha kupoza na kuzambaza umeme cha Zuzu.
Katika kikao hicho, mambo
mbalimbali yalijadiliwa kuhusiana na nishati ya umeme inayozalishwa
nchini kwa lengo la kuleta manufaa makubwa zaidi kiuchumi kwa nchi,
Shirika na watumiaji wa umeme huo ikiwemo viwanda, wafanyabiashara na
matumizi mengine.
Dkt. Kalemani aliiagiza TANESCO,
kulipa madeni yote inayodaiwa na kutoongeza madeni mapya, vilevile
wadaiwa sugu wakumbushwe madeni yao,na endapo hatawalipa, TANESCO
iwakatie umeme, kwa kufanya hivyo kutamaliza tatizo la wadaiwa sugu.
“TANESCO inadaiwa madeni makubwa,
pia ina wateja wengi sana ambao ni wadaiwa sugu wanaodaiwa fedha nyingi
sana na hawalipi ,zimo Taasisi, Mashirika ya Umma na binafsi, pamoja na
watumiaji wa kawaida, ninawaagiza nendeni mkawakatie umeme! narudia tena
mkakate umeme! mkishaukata, wahusika watalipa na wataonyesha
ushirikiano mkubwa, tofauti na kumdai kawaida tu”, alisema Dkt.
Kalemani.
Kuhusu wizi na uhujumu wa
miundombinu ya umeme, Dkt. Kalemani, aliitaka TANESCO, Bodi ya TANESCO
na Watendaji wa Wizara ya Nishati, kushirikiana kwa pamoja kutafuta njia
sahihi naya kisasa zaidi ya kubaini wizi wa umeme,unaofanywa na watu
wasiowaaminifu na kusababisha hasara kwa shirika na kupoteza mapato ya
taifa.
“Wizi wa umeme upo na haukubaliki,
tuweke mfumo sahihi wa kisasa kubaini wahusika, tuache na hii tabia ya
kukimbizana kimbizana na wezi, pia sisi watumishi tuwe wazalendo,na
wasimamizi wazuri wa miundombinu yetu,vilevile tuwe na walinzi wenye
weledi katika miradi yetu bila kujali niya serikali au mtu binafsi,
jukumu la ulinzi ni letu sote faida ya Taifa kwa jumla”,alisisitiza Dkt.
Kalemani.
Aidha aliwataka kuendelea kufanya
tathmini na uwiano wa gharama za kutengeneza nguzo za Zege na nguzo
zinazotumika sasa,ili kuangalia uwezekano wa kutumia nguzo za zege
katika maeneo yote nchini lakini kwa gharama nafuu, kwa lengo la
kukabiliana na changamoto ya kuoza ama kuungua kwa nguzo katika maeneo
mbalimbali.
Hata hivyo aliweka wazi kuwa
katika baadhi ya maeneo machache ambayo ni korofi nguzo za zege zimeanza
kutumika japo ni za gharama kubwa.
Vilevile alitaka kuongezeka kwa
idadi ya wateja wa umeme katika kila sekta, kuharakisha uunganishaji wa
umeme kwa mteja pale anapomaliza kulipia gharama husika, pamoja na
kutatua changamoto za wateja kwa wakati sahihi ili kuvutia wateja wengi
zaidi na kuondoa malalaliko.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu aliwataka TANESCO kuangalia uwezekano wa kutoa
zawadi kubwa kwa wasamaria wema wanaotoa taarifa za siri kuhusu
wanaohujumu na kuiba umeme tofauti na ile inayotolewa sasa, ambayo pia
huchukuwa muda mrefu kuikabidhi kwa mhusika.
Mgalu alikitaka kitengo husika
kitunza siri za watoa taarifa,pia kifanye uchunguzi wa kina na kutoa
adhabu kwa mtumishi yeyote atakayetiliwa shaka, au kuhusika na wizi
pamoja na kuhujumu miundombinu ya umeme kama inavyofanywa kwa wahisika
wengine wanaobainika.
Vilevile kuwe na uhamasishaji wa
kuwavutia watoa taarifa ili kupata matokeo chanya kunusu wizi na uhujumu
wa miundombinu ya umeme nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Mhandisi Zena Said, alieleza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya wizi
na uhujumu wa miundombinu ya umeme, watashirikiana na Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) kuimarisha ulinzi
kuanzia ngazi za Kaya.
Mhandisi Said, alisema kwa kufanya
hivyo kutasaidia sana kubaini wezi na wahujumu miundombinu ya umeme kwa
kuwa watu hao wasio wazalendo huwa wanaoneka na hata kufahamika katika
maeneo yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, aliishuruku Wizara ya Nishati kwa kuwapa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na kuyafanyia kazi yale waliokuwa wakiishauri wizara hiyo, katika kipindi chote cha miaka mitano
Dkt.Kiyarunzi, alikiri kwa kuwa
kazi ya kusambaza umeme si jambo jepesi, hivyo wanajivunia kuona
maendeleo makubwa katika sekta ya nishati ya kuongeza wigo wa usambazaji
wa umeme vijijini, kujenga miradi mikubwa ya kuzalisha, njia za
kusafirisha na kusambaza umeme pamoja na vituo vya kupoza na kusambaza
umeme nchini.
Awali kabla ya kufanyika kwa kikao
hicho, Uongozi wa Wizara na Wajumbe wa Bodi hiyo walifanya ziara ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa Kituo kikubwa zaidi nchini cha
Kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Dkt. Kalemani,
ujenzi wa kituo hicho utakamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Mei, 2020 na
kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 648 tofauti na vituo vingine.
Na kituo hicho kitaimarisha
upatikanaji wa umeme kwa Jijiji la Dodoma ambalo linaendelea kukuwa kwa
kasi na kitakuwa ndiyo kitovu cha vituo vyote vya kupoza kuzambaza
umeme katika mikoa yote nchini na kuupeleka nchi jirani pale
itakapohitajika kufanya hivyo.
No comments :
Post a Comment