Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (mwenye kofia mbele)
akiingia ndani ya kiwanda cha Exel Chemical Ltd. kilichopo wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kufanya ukaguzi kufuatia malalamiko
ya wadau mbalimbali kuhusu uchafuzi wa mazingira. Hata hivyo uchunguzi
unaendelea kuhusu tuhuma za kufanya kazi bila leseni na kukwepa kodi.
Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akikagua nyaraka
mbalimbali za kiwanda cha Exel Chemical Ltd. cha wilayani Bagamoyo
kinachodaiwa kukiuka taratibu mbalimbali zikiwemo jina la bidhaa
kutofautiana na jina la kiwanda pamoja na uchafuzi wa mazingira ikiwemo
kelele na vumbi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akingalia shehena ya
mifuko ya unga wa kutengenezea rangi kutokana na mawe yaliyosagwa
ambapo bidhaa hiyo imeandikwa Watercraft tofauti na jina la kiwanda la
Exel Chemical Ltd. jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa maelekezo kwa
viongozi mbalimbali alipofanya ziara katika kiwanda cha kusaga mawe cha
Exel Chemical cha wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambapo ilibainika
kiwanda hicho kinatumia jina tofauti na la bidhaa inayozalisha huku
Serikali ikiendelea na uchunguzi na tuhuma za kufanya kazi bila leseni
wala kulipa kodi.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu ameiagiza Wilaya ya
Bagamoyo mkoani Pwani kufanya uhakiki wa viwanda vyote
vilivyopo
wilayani hapa kubaini endapo vinaendeshwa kihalali au la.
Zungu ametoa agizo hilo leo
wilayani hapa alipofanya ziara ya kukagua kiwanda cha Exel Chemical Ltd.
kinachojishughulisha na kusaga mawe kwa ajili ya kutengenezea rangi
kufuatia malalamiko kutoka kwa wadau wa mazingira pamoja kufanya zake
shughuli kinyume cha taratibu.
Alisema kuwa Serikali inachunguza
kubaini kiwanda hicho kinavyofanya shughuli zake kama inalipa kulipa
kodi au leseni na kama wakibaini hailipi kodi hatua stahiki
zitachukuliwa.
Katika ziara hiyo akiwa
ameambatana na viongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) uongozi wa Wilaya hiyo Zungu alibaini jina la kiwanda
ni Exel Chemical wakati bidhaa inayozalishwa ni Watercraft jambo ambalo
linakwenda kinyume cha sheria.
Aidha, waziri huyo alisisitiza
kuwa nchi inataka wawekezaji katika sekta ya viwanda wafanye kazi bila
kubughudhiwa wala kuonewa na wala Serikali haitafunga kiwanda lakini
sharti lazima wafuate sheria za nchi zikiwemo za mazingira.
“Viwanda hivi vinafanya kazi bila
leseni na wakifanya hivi Serikali inakosa mapato, na Serikali ikikosa
mapato halmashauri mtakosa ‘on source’ za kuendesha shughuli zenu sasa
fanyeni auditing kubaini viwanda gani viko kihalali na vipi vipo
kiharamu ili sasa tuanze kuchukua hatua ili walipe leseni kwa mafunfaa
ya Taifa,” alisema Zungu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NEMC
Dkt. Samuel Gwamaka alisema kuwa imebaini kiwanda hicho ambacho kipo
karibu na makazi ya watu kinafanya shughuli zake kinyume cha taratibu za
mazingira.
Dkt. Gwamaka alibainisha kuwa
kutokana na ukaguzi uliofanyika imebainika kuwa kiwanda hicho kimekuwa
kikichafua hewa kwa kutoa vumbi na kuwa ni chanzo cha kelele jambo
ambalo linatishia afya za wakazi wa eneo hilo.
Hata hivyo bado uchunguzi kuhusu
tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi ya kiwanda hicho unaendelea ili
kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki kwa mmiliki huyo.
Aidha Serikali kufuatia tuhuma
hizo inaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini ni jina gani halisi la
usajili wa kiwanda hicho pamoja na mwenendo mzima wa ulipaji kodi,
No comments :
Post a Comment