Wednesday, April 8, 2020

WAFANYA BIASHARA WAMETAKIWA KUWA WAVUMILIVU KUKAMILISHIWA MFUMO WA UPATIKANAJI WA FOMU ZA MAOMBI MTANDAONI



Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na Wandishi wa habari leo ofisini kwake wakati akitangaza mfumo mpya wa kujaza fomu za kuomba kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati kwenye jiji hilo.
…………………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna,Dodoma
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewataka wafanya biashara wa wanaotaka kuwekeza katika miradi ya kimkakati iliyoko jijini Dodoma kuwa na Subira ili
kukamilisha mfumo wa uaptikanaji wa fomu kwenye mtandao.
Wito huo ameutoa  leo jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya kuweka utaratibu maalum wa upatikanaji wa fomu za maombi ya kufanya biashara katika miradi ya kimkakati iliyoko jijini Dodoma.
Kunambi amesema kuwa ameunda timu ya wataalamu kutoka sehemu mbali mbali ili kuanda mfumo huo utakao muwezesha kila mtanzania anayetaka kufanya biashara katika miradi hiyo kuweza kupata fomu mtandaoni.
“Lengo letu la kuweka utaratibu huu ni kuepusha msongamano husiokuwa na lazima, safari zisizo za lazima ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhali ju ya janga la corona kama mnavyo jua taifa na dunia kwa ujumla tuko katika mapambano dhidi ya janga hili”, ameeleza Kunambi.
Aidha Kunambi ameweka wazi kuwa kuja kufikia Jumatatu ya wiki ijayo wataalmu wake watakuwa wamekamilisha mfumo huo wa upatikanaji wa fomu hizo na watanzania watapatiwa maelekezo namna ya upatikanaji wa fomu hizo katika mtandao.
Akizungumza Kunambi amesema kuwa mfumo huo utasaidia kurahisisha upatikanaji wa fomu hizo na kuondoa kauli za tuhuma kwa viongozi wake kuwa hawakutenda haki katika utoaji wa nafasi hizo za kufanyia biashara.
Kunambi ameongeza kuwa fomu hizo zitapatikana kwa kiasi cha shilingi 20,000/= na baada ya muda uliyopangwa ndani ya siku saba baada ya kuanza kuchukua fomu hizo wataalamu wake watakaa na kupitia fomu hizo kwa umakini na kuzifanyia kazi kwa haraka ili watanzania waweze kunufaika na miradi iliyojengwa kwa kodi zao.
Aidha Kunambi ametoa onyo kali kwa watu ambao si wafanya biashara wanao taka kuwa madalali katika zoezi hili kuwa hawatakuwa na nafasi ya kufanya ujanja wowote kwa timu inayoratibu zoezi hilo imekamilika kwa kuwa na wataalamu kutoka kila idara wakiwemo watu wa TAKUKURU .

No comments :

Post a Comment