Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa
Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN) Bruno
Ghumpi (mwenye shati la batiki) akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa uwepo
wa elimu kwa wazazi na walezi ili kuwaelimisha watoto kuhusu kujikinga
na maambukizi ya Virusi vya Corona katika kikao kilichofanyika jijini
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Iadara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Mathias Haule akichangia hoja
katika kuandaa ujumbe utakaowalenga wazazi kuwaelimisha watoto jinsi ya
kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona katika kikao kilichofanyika
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau
wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao kilichowakutanisha Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii kwa lengo la kuandaa ujumbe utakaowalenga wazazi kuwaelimisha
watoto jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
*******************************
Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii) kwa kushirikiana na Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya
Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN), Taasisi ya Chakula na Lishe, Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) wameandaa mkakati wa
kufikisha ujumbe kwa watoto kuhusu kujikinga na maambukizi ya Virusi
vya Corona.
Akizungumza leo
katika kikao kazi kilichowakutanisha wadau hao jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Watoto
Wadogo Tanzania (TECDEN) Bruno Ghumpi amesema kumekuwepo na ujumbe
mbalimbali katika kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona ila
kumekosekana ujumbe maalum unaolenga makundi maaalum ikiwemo wanawake
wajawazito na watoto wadogo kuanzia miaka 0 hadi minane.
Ameongeza kuwa
kuwepo kwa elimu sahihi kwa watoto hao kuhusu ugonjwa wa COVID 19
itawasaidia wazazi au walezi na watoto wenyewe kupata taarifa
zitakaziwasaidia kujikinga na Virusi hivyo ili kupunguza au kuondokana
na maambukizi ya Virusi hivyo katika maeneo yao.
“Ujumbe huu kwa
watoto ni muhimu sana kwani kundi hili kwa sasa lipo nyumbani kutokana
na kufungwa kwa shule hivyo ni vizuri wazazi na walezi wakazingatia
masuala muhimu ya kuwafundisha watoto wao kujikinga na maambukizi ya
virusi vya Corona” amesema
Kwa upande wake
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Mathias
Haule amesema kuwa ni muhimu kwa wadau kuhakikisha wanafikisha elimu
katika ngazi ya chini kuanzia familia, kijiji/mtaa ili kuwezesha watu
hao kupata taarifa na elimu sahihi juu ya kujikinga na maambukizi ya
virusi vya Corona.
“Elimu ifike
katika ngazi ya familia hasa katika maeneo ya vijijini ambako bado elimu
haijawafikia kwa kasi inayotakiwa ili kuondokana na maambukizi ya
virusi vya Corona nchini.” Amesema
No comments :
Post a Comment