Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (katikati) akitoa
maelekezo kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha
Paulsen(hayupo pichani) kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anamlipa
mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ya Bongo Star Search kwa mwaka 2019
Bw.Meshack Fukuta, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) Aprili
08,202 Jijini Dodoma,kulia ni Afisa Utamaduni Bw.Mfaume Said kutoka
hiyo na kushoto ni Mshindi wa kwanza wa shindano la Bongo Star Search
mwaka 2019 (BSS) Bw.Meshack Fukuta.
Mshindi wa kwanza wa shindano la
Bongo Star Search (BSS) la mwaka 2019 yanayoendeshwa na Kampuni ya
Benchmark Production Bw.Meshack Fukuta, akitoa ufafanuzi kuhusu kiasi
cha pesa alicholipwa kama zawadi aliyoahidiwa kuwa ni shilingi milioni
moja na siyo milioni mbili kama inavyoelezwa katika mkutano wa Naibu
Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
nawaandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kulia) akitoa maelekezo
kwa Mkurugenzi wa Benchmark Production Madam Ritha Paulsen kuhakikisha
ndani ya mwezi mmoja anamlipa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Bongo
Star Search wa mwaka 2019 Bw.Meshack Fukuta, mbele ya waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo Aprili 08,202 Jijini Dodoma, na kushoto ni
Mshindi wa kwanza wa Shindano la Bongo Star Search mwaka 2019 (BSS)
Bw.Meshack Fukuta.
Baadhi ya waaandishi wa Habari
wakifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza kwa Mkurugenzi wa Benchmark
Production Madam Ritha Paulsen (hayupo pichani) kuhakikisha ndani ya
mwezi mmoja anampatia mshindi wa kwanza wa mashindano Bongo Star Search
ya mwaka 2019 zawadi yake ya milioni 50 leo Aprili 08,202 Jijini
Dodoma.
……………………………………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma.
Uongozi wa Kampuni ya Benchmark
Production chini ya Mkurugenzi wake Madam Rita Paulsen inayoendesha
Mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama
Bongo
Star Search (BSS) umepewa siku saba uwe umeripoti Wizara ya Sanaa,
Michezo na Utamaduni ili kuweza kuweka wazi ni lini watakamilisha
stahiki za mshindi wa shandano hilo wa mwaka 2019.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Waziri wa Sanaa,Michezo na Utamaduni Juliana Shonza leo wakati
akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kupokea
barua kutoka kwa familia ya mshindi huyo iliyoeleza kutokutekelezwa kwa
ahadi hiyo kwa takriban miezi minne sasa ilioanisha utaratibu wa malipo
hayo kuwa milioni 30 ni kwa ajili kutengeneza kazi za muziki na
matangazo kwa kipindi cha mwaka mmoja na milioni 20 ni ya kukabidhiwa
mkononi ambapo Mhe. Naibu Waziri amesisitiza makubaliano yote
yalioanishwa kufanyiwa kazi.
Shonza amesema kuwa Kiongozi wa
BSS anatakiwa kufika katika ofisi za wizara ili kujadili mpango kazi wa
viongozi hao watakavyo mmaneji kijana huyo katika fedha ya kiasi cha
milioni 30 ili mpango kazi huo uwezekuendana na kiasi cha fedha
alizostaili kupata ikiwemo na kuangalia utaratibu wa malipo yake
yatakavyo kamilishwa.
Shonza amesema kuwa maelekezo hayo
yanakuja baada ya kupokea malalamiko kutoka katika familia ya mshindi
huyo na kumsikiliza muhusika mwenyew ambaye hakupewa stahiki zake mpaka
leo na tumejilidhisha kuwa kuna makosa ya kisheria yamefanyika na BSS
waandaji wa shindano hilo.
“Baada ya kusikiliza pande zote
tatu muandaji, mdhamini na mshindi BSS ndani ya siku 30 wawe
wamekamilisha stahiki za kijana Meshaki Fukuta ili aweze kuendelea
katika kukuza kipaji chake kwani sisi kama serikali ni kulinda haki za
wasanii na kuwawezesha kufikia malengo yao katika kutafuta haki zao”
ameeleza Shonza.
Shonza amesisitiza kuwa BSS ndani
ya mwezi mmoja Wakifanya vinginevyo mashindano hayo yatafungiwa kama
watakuwa hawajamlipa ndani ya muda huo.
Katika hatua nyingine Shonza
ametoa wito kwa wa Wasanii kuwa wasikubali kufanya kazi bila mkataba ili
kuwa rahisi kuweza kupata sitahiki zao kwa wakati na kuwataka BASATA
kukagua mikataba ya washiriki katika mashindano kabla ya kutoa kibali
cha kuendesha shindano lolote.
Lakini pia Shonza ameongeza kuwa
waandaaji wa mashindano waandae zawadi za uhalisia ili kuwa rahisi
kuendesha mashindano hayo ili kufanyikisha lengo la kumuinua kijana
kufikia malengo yake na kuepuka changemoto kama hizi zilizo jitokeza kwa
kijana Bw.Meshack Fukuta.
Naye Mshindi wa BSS 2019
Bw.Meshack Fukuta amesema kuwa amekuwa akifatilia zawadi yake yenye
ghalama ya kiasi cha shilingi milioni 50 lakini hakufanyikiwa kupata
kutokana na uongozi wa BSS kumpiga tarehe kila alipokwenda katika ofisi
zao.
Ikumbukwe hivi karibuni changamoto
kama hiyo ilijitokeza katika shindano la Miss Tanzania ambapo tatizo
hilo lilipelekea mwendesha mashindano hayo kufungiwa na shindano hilo
kupewa mtu mwingine
No comments :
Post a Comment