******************************
–Vitagawiwa bure kwenye vituo vya afya na kwa wananchi
Katika kuunga
mkoni jitihada za Serikali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa
COVID-19, Kampuni ya bia Tanzana (TBL Plc) kwa kushirikiana na kampuni
ya Diversey East and Central Africa Limited, imeanza kuzalisha vitakasa
mikono kwa kutuma malighafi zenye kilevi.
Mkurugenzi Mkuu
wa TBL Plc, Philip Redman, amesema kampuni yake itatoa msaada wa lita
681 za vitakasa mikono zikiwa kwenye vifungashio vya lita 5 kwa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ajili ya kutumiwa
kwenye vituo vya afya nchini pote.
Redman,
aliongeza kusema kulinda afya na usalama kwa wafanyakazi wa TBL Plc na
familia zao nchini kote, wateja wake na jamii nzima kwa ujumla ni suala
ambalo kampuni inalipa umuhimu mkubwa. Alishukuru ushirikiano iliopata
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya
Viwanda na Biashara na kampuni ya Diversey kwa kufanikisha mchakato huu
wa kuzalisha bidhaa za vitakasa mikono kwa lengo la kuunga
mkono jitihada za serikali katika kupambana na ugonjwa wa COVID- 19.
Mbali na
kuzalisha vitakasa mikono kwa ajili ya vituo vya afya nchini, TBL
itazalisha lita 6,180 katika vifungashio vya mililita 500 kwa ajili ya
kuwagawia wateja wake na kwenye jamii sehemu mbalimbali nchini. Vitakasa
mikono hivyo ambavyo vimetengenezwa kwa malighafi yenye kilevi ya
Ethanol, maji na glycerin vitagawiwa bure sio kwa ajili yake biashara na
vina viwango vinavyokubalika na maelezo kuhusiana na matumizi yake.
TBL ina historia ndefu ya kusaidia kukuza uchumi wa kijamii nchini Tanzania kupitia sekta ya kilimo, usafirishaji na viwanda.
No comments :
Post a Comment