Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa
dini kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini
katika Mkutano uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea jinsi Wizara
inavyoshirikiana na wadau katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi
vya Corona katika Mkutano kati ya Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)
na viongozi wa Dini jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la World
Vision Gilbert Kamanga akielezea jinsi Shirika hilo linavyoshirikiana na
Serikali katika mapambano dhidi maambukizi ya Virusi vya Corona katika
Mkutano kati ya Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini
jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya
viongozi wa kidini wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika
Mkutano kati yao na Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu WAMJW Dar es Salaam
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema
Tanzania imeanza kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ya ndani kuanzia
maambukizi yaliyopatika tarehe 08/04/2020.
Amesema kuwa
tahadhari kubwa inahitajika katika kuhakikisha kuzuia kuendelea kwa
maambukizi ya kijamii itasababisha kuongezekana kwa kasi ya maambukizi
katika jamii.
Ameyazungumza
hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na viongozi wakuu wa
madhehebu ya dini katika kujadiliana namna ya kukabiliana na maambukizi
ya virusi ya Corona nchini.
Ameongeza kuwa
Serikali itatangaza hivi karibuni wananchi kuchukua tahadhari kwani
tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaweza kusambaa na kuambukizwa kwa
njia ya hewa hivyo maelekezo ya kutumia barakoa yatatolewa ili
kuondokana na maambukizi.
“Tafiti
zimeonesha kuna uwezekano wa Virusi vya Corona vinaweza kuenezwa kwa
njia ya hewa hivyo tutaleta muongozo wa kuanza kutumia Barakoa (Mask)
kwa jamii ili kuziua maambukizi kuenena kwa njia ya hewa” alisema
Aidha amewataka
viongozi wa dini kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwalinda watoto
kutowaruhusu Watoto kuzurula na kuhangaika ovyo mitaani ili kupunguza
uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
“Imani ya
watanzania wengi kufikiri kuwa hatuwezi kupata maambukizi ni suala
sahihi tunaweza kupata maambukizi kama watu wengine wanavyopata”
alisema.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa viongozi ni
watu muhimu katika kuleta mabadiliko katika Jamii yetu kwani
wanasikilizwa zaidi na waumini katika sehemu za ibada.
Ameongeza kuwa
lengo ni kuwashirisha viongozi wa kidini katika kuhakikisha wanatimiza
wajibu wao katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Corona
yanatokomea nchini.
“Viongozi wa
kidini ni watu muhimu sana katika mapambano katika kuondokana na
maambukizi ya Virusi vya Corona nchini tunaomba mtusaidie katika hili”
alisema
Naye Mkurugenzi
wa Shirika la World Vision Gilbert Kamanga amewaomba vingozi wa dini
kutofanya suala la virusi vya Corona kuwa la kisiasa bali waunganishe
nguvu pamoja ili kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Ameongeza kuwa
jamii inatakiwa kupewa elimu kila mahali ikiwemo katika nyumba za ibada
ambapo watu wengi ukusanyika pamoja kuabudu itakuwa sehemu sahihi
kufikisha ujumbe kuhusu kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
“Viongozi wetu wa
dini nawaomba tushikamane katika hili kwani virusi vya Corona ni hatari
sana lakini tukisimama pamoja hakika tutafanikiwa katika kutokomeza
virusi vya Corona” alisema
Akitoa salam za
mkoa wa Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rashid Mfaume amesema
mkoa umejidhatiti katika kupambana kwa kuenea na maambukizi ya Virusi
vya Corona mkoani humo kwa kuzingatia maelekezo yanayotokea na wataalam
wa Afya na Serikali kwa ujumla.
Naye Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Musa Salum amesema janga la Corona ni
kubwa na kama watu wa imani tunaamini katika kumuonba Mwenyezi Mungu na
tunaamini litatokomea.
Pia amemshukuru
Rais John Magufuli kuendelea kuruhusu ibada kuendelea katika kama
kawaida ni jambo ambalo litasaidia kuzidisha maombi katika kupambana na
Virusi vya Corona.
Mkutano huu kati
ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini umekuja wakati Tanzania
ikiendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona huku ikiwa na
jumla ya watu 25 waliombukizwa virusi hivyo.
No comments :
Post a Comment