Friday, April 10, 2020

BRIGHTER MONDAY TANZANIA YAZINDUA KAMPENI YA ‘UMOJA WAKATI WA SHIDA’ KUSAIDIA WAAJIRI KUKABILIANA NA ATHARI ZA JANGA LA CORONA



……………………………………………………………………………………….
Kampuni ya uajiri na usimamizi wa rasilimali watu ya BrighterMonday Tanzania imeanzisha programu iitwayo ‘Umoja Wakati wa Shida’ inayotoa nafasi kwa waajiri (makampuni na watu binafsi) kutangaza kazi kwenye tovuti yao bure kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo, wakati
ambao taifa linakabiliana na janga la maradhi ya virusi vya Corona.
Kampeni hii inalenga kuwezesha uendelevu wa juhudi za makampuni na biashara kwa kuziwesesha kufanya udahili na kuajiri watendaji sahihi ili kuongeza ufanisi wakati na baada ya nyakati hizi za changamoto.
‘’Kwa miezi mitatu ijayo, tutatoa fursa kwa taasisi zinazotaka kuajiri wataalamu katika sekta mbalimbali kote nchini kutangaza bure nafasi za ajira katika tovuti yetu. Hii itawawezesha hospitali, vituo vya afya na watoa huduma nyingine muhimu walio mstari wa mbele katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona (COVID-19) kuajiri wataalamu wenye vigezo kamilifu katika kipindi cha muda mfupi’’, anasema Mkurugenzi Mkuu wa BrighterMonday Tanzania, Bi. Reshma Bharmal-Shariff.
Chini ya programu hii, waajiri wataweza kuchakata kwa haraka mchakato wa uajiri kwa kutumia mbinu za kisasa zilizobuniwa na BrighterMonday Tanzania kama vile Zana ya Kupima Ufanisi wa Waajiriwa ambayo inapima ubora wa mwajiriwa na ujuzi unaohitajika kwa kazi anayoomba, zana hii hupima zaidi ya kile kilichopo kwenye wasifu (CV) ya mtahiniwa.
Vilevile, waajiri wataweza kuangalia alama za mtahiniwa pamoja kulinganisha na mahitaji ya kitaaluma na kiuzoefu kwa kutumia mfumo wa ufuatilaji wa maombi ya kazi ‘Application Tracking System’ (ATS) wa BrighterMonday Tanzania. Kupitia mfumo huu, mwajiri ataweza kulinganisha kwa urahisi ubora wa mtahiniwa, ujuzi na kiwango cha uzoefu.
‘Tupo kwa ajili yako jana, leo na hata kesho’- Timu ya BrighterMonday Tanzania inasema.
Kuhusu BrighterMonday Tanzania
BrighterMonday Tanzania ilianzishwa mwaka 2012 na kwa sasa imekuwa moja ya jukwaa linaloongoza kwa uajiri na usimamizi wa huduma za rasilimali watu. Jukwaa letu lina zaidi ya watu 140,000 waliojiunga kutafuta fursa mbalimbali za ajira na zaidi ya waajiri 2,000 wanaotafuta waajiriwa sahihi.
Maono yetu ni kuwa chanzo kinachoongoza cha kutoa vipawa kwenye soko la ajira kwa kuwapatia waajiri na watafutaji kazi jukwaa linalorahisisha utafutaji wa kazi na upatikanaji wa wataalamu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na;
Erca Uisso | + 255 659 540 772 | ercau@brightermonday.co.tz
Dar es Salaam, April 08, 2020 – “ Recruitment firm BrighterMonday Tanzania has launched an initiative
dubbed ‘Unity In Adversity’ that offers free job listing services for individuals or companies seeking to hire as the country battles Coronavirus (COVID-19).
The campaign seeks to boost the continuity of businesses efforts by enabling organisations to recruit the right people to steer them during and beyond the current challenging times.
“For the next three months, we will give organizations seeking to recruit professionals across different industries countrywide free job listings on our website. This will enable county hospitals, healthcare facilities and other essential services providers at the frontline in the fight against COVID-19 to hire qualified candidates in the shortest time possible,” said Mrs. Reshma Bharmal-Shariff, Chief Executive Officer, BrighterMonday Tanzania.
Under the initiative, employers will be able to fast track the recruitment process with some of
BrighterMonday’s innovative products like the firm’s newly launched proficiency Assessment Tool that tests a candidate’s core competencies and hard skills required for a specific role beyond what is captured on their CVs during the hiring process.
Additionally, hiring managers will be able to view a candidate’s scores alongside other filters like
education and experience levels with the use of BrighterMonday’s Applicant Tracking System (ATS), a back-end filter that augments the Assessment Tool. This way they will be able to compare a candidate’s proficiency, qualifications and experience levels at a glance.
Here for you yesterday, today and tomorrow.” says BrighterMonday Tanzania team.
////
About BrighterMonday Tanzania
BrighterMonday Tanzania was established in 2012 and has grown to become one of Tanzania’s leading
recruitment and HR services platform. We have over 140,000+ candidates and 2,200+ employers,
successfully using the platform to get access to the right opportunities.
Our vision is to be the leading source of talent in our markets by providing a platform through which Job
search and talent acquisition are simplified.
For more information, please contact:
Erca Uisso | + 255 659 540 772 | ercau@brightermonday.co.tz

No comments :

Post a Comment