Mkurugenzi wa TBL Plc
, Philip Redman, ( wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa
tani 9 za unga wa mahindi zilizotolewa na kampuni hiyo kwa Mbunge wa
jimbo la Rufiji mkoa wa Pwani , Mohamed Mchengerwa , kwa ajili ya
wahanga wa mafuriko yaliyotokea Rufiji hivi karibuni, hafla hiyo
makao makuu ya kampuni Ilala jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha
ni wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa TBL Plc
, Philip Redman, akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi
msaada wa tani 9 zilizotolewa na kampuni kwa wahanga wa mafuriko
yaliyotokea Rufiji hivi karibuni.
…………………………………………………………………………
Kampuni ya Tanzania
Breweries Public Limited Company,imetoa msaada wa tani 8.75 za unga wa
mahindi kwa wahanga wa mafuriko ya mvua kubwa huko Rufiji iliyonyesha
hivi
karibuni na kusababisha maafa makubwa.
Msaada
huo umekabidhiwa kwa Mbunge wa Rufiji, Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa,
kwa ajili ya kuwapatia unafuu wa maisha wakazi hao ambao nyumba zao
zaidi ya 3,500 na hekari 6,600 zilisombwa na mafuriko katika mkoa wa
Pwani.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa TBL Plc,Philip
Redman alisema “Sisi kama TBL Plc, tumejitoa kusaidia jamii
tunayofanyia biashara zetu na hii ni moja ya njia yetu mojawapo ya
kurudisha tunachokipata kwao hususani kipindi ambacho wanahitaji
msaada.”
Kwa upande wake, Mheshimiwa
Mchengerwa, alitoa shukrani kwa msaada huo kutoka TBL Plc na kutoa wito
kwa taasisi nyinginezo na watu binafsi kusaidia wahanga hao wa mafuriko
kulingana na uwezo wao.
TBL Plc ina historia ya kusaidia
kuendeleza uchumi wa kijamii nchini Tanzania kupitia sekta za kilimo,
usafirishaji na viwanda. Kwa upande wa sekta ya kilimo, kampuni imekuwa
ikinunua mazao ya Shahiri,mahindi,mtama na zabibu kwa ajili ya malighafi
ya kuzalisha bidhaa zake. Mwaka jana kampuni ilinunua zaidi ya tani
20,000 za malighafi ya nafaka kutoka hapa nchini.
No comments :
Post a Comment