Mwenyekiti wa Tume ya Madini,
Profesa Idris Kukula (kushoto) akiongoza kikao cha kazi cha Tume ya
Madini kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 15 Aprili, 2020. Kulia ni
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya.
Katibu Mtendaji wa Tume ya
Madini, Profesa Shukrani Manya (kulia) akielezea mafanikio ya utendaji
wa majukumu ya Tume ya Madini kwenye kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti
wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kukula.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo, akichangia mada kwenye kikao hicho.
Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt.
Athanas Macheyeki akielezea namna Tume ya Madini inavyosimamia
utekelezaji wa mipango ya ushirikishwaji wa wazawa kwenye Sekta ya
Madini kwenye kikao hicho.
Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi na
Biashara ya Madini wa Tume ya Madini, George Kaseza akielezea mikakati
ya Tume kwenye usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa
madini nchini.
Kutoka kushoto mbele Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo na Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa wakifuatilia
ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini,
Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani)
Kutoka kushoto mbele Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo na Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa wakifuatilia
ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini,
Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani)
Watendaji kutoka Tume ya Madini wakifuatilia majadiliano mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea katika kikao hicho.
………………………………………………….
Leo tarehe 15 Aprili, 2020
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ameongoza kikao cha
kazi cha Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma lengo likiwa ni
kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa
kipindi cha robo mwaka.
Kikao hicho kimeshirikisha
Makamishna wa Tume ya Madini ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo, Katibu Mkuu wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.
Makamishna wengine ni pamoja
na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini
Tanzania (FEMATA), Haroun Kinega, Prof. Abdulkarim Mruma na Dkt. Athanas
Macheyeki.
No comments :
Post a Comment