********************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni
476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane mkoani humo ambao nyumba
zao zimeathiriwa na
mafuriko yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha
ambapo amewataka Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka.
RC Makonda amesema hayo wakati wa
Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane
ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto
ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo
ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha
waliyoipata.
Aidha RC Makonda amewapa siku 10
Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua
athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa
ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti
ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.
Aidha RC Makonda amesema athari
zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu
wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba
mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila
mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema
kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja
yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili
kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.
RC Makonda pia amewaelekeza
wakandarasi kutumia kipindi hiki cha mvua kuangalia kama Design ya
madaraja wanayojenga yanakidhi kuhimili na kupitisha maji ya mvua ili
wabuni design mpya zinazokidhi viwango.
No comments :
Post a Comment