Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifuatilia wadaiwa wa kodi ya
pango la ardhi katika mfumo wa kielektroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za
wamiliki wa ardhi katika halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu
juzi akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi.
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi wizara ya Ardhi Denis Masami.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizingumza na Wakurugenzi na
Watendaji wa sekta ya rdhi katika halmashauri za mkoa wa Simiyu juzi
akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi.
Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga na wa
tatu kulia ni Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Simiyu Maganga Simon.
Watendaji wa sekta ya ardhi katika
halmashauri za mkoa wa Simiyu wakiwemo Wakurugenzi wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
(hayupo pichani) alipofanya ziara kukagua utendaji kazi wa sekta ya
ardhi katika mkoa huo juzi.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoani
Simiyu Festo Kiswaga akizungumza wakati wa kikao baina ya Watendaji wa
sekta ya ardhi wa halmashauri za mkoa wa Simiyu na Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara ya
kukagua utendaji kazi wa sekta ya rdhi katika mkoa huo juzi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi vifaa kwa ajili ya
kurahisisha ukusanyaji kodi ya pango la ardhi Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu Melkizedek Oscar wakati alipofanya ziara
ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa huo juzi.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Denis Masami (PICHA
ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)
……………………………………………………………………………………………
Na Munir Shemweta, WANMM SIMIYU
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka
wamiliki wa ardhi wanaotaka kilipia kodi ya pango la ardhi kufanya hivyo
kupitia mitandao ya
simu za viganjani ili kuepuka misongamano inayoweza
kuchangia maambukizi ya virusi vya Corona.
Dkt Mabula alitoa
tahadhari hiyo juzi wilayani Bariadi mkoani Simiyu alipozungumza na
Wakurugenzi na Watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa
Simiyu akiwa katika ziara ya kuangalia utendaji kazi wa sekta hiyo
sambamba na kufautilia maagizo aliyoyatoa kuhusiaa na sekta ya ardhi.
Alisema, ni
vizuri katika kipindi hiki ambacho kuna maambulizi ya virusi vya Corona
wamiliki wa ardhi wakachukua tahadhari ya kutokwenda ofisi za ardhi
kulipia kodi ya pango la ardhi na badala yake wafanye malipo kwa kutumia
mitandao ya simu.
Kwa mujibu wa
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, malipo ya kodi ya
pango la ardhi yanaweza kufanyika kwa kutumia mitandao yote ya simu za
viganjani pamoja na kutembelea tovuti ya Wizara.
‘’Katika kipindi
hiki ambacho kuna maambukizi ya virusi vya Corona wadaiwa pamoja na wale
wanaotaka kilipia kodi ya pango la ardhi wakafanya hivyo kupitia
mitandao ya simu pamoka na kutembelea tovuti ya Wizara ili kuepuka
misongamano inayoweza kuchangia maambukizi’’ alisema Dkt Mabula
Akigeukia suala
la makusanyo ya kodi ya Pango la Ardhi katika halmashauri za mkoa wa
Simiyu, Dkt Mabula ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ya ukusanyaji kodi
ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Simiyu pamoja na mkoa huo
kusifika katika masuala ya uwekezaji.
‘’ Mkoa wa Simiyu
mapato yatokanayo na kadi ya pango la ardhi yako chini sana, lengo la
makusanyo kwa mkoa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 ni kukusanya
bilioni 10 lakini kiasi mlichokusanya hadi sasa ni milioni 190 tu sawa
na asilimia 9.1, inaonesha hamjawa makini kufuatilia madeni’’ alisema
Dkt Mabula
Aidha, Naibu
Waziri Mabula alisema hata malengo ya makusanyo ya kodi ya pango la
ardhi yaliyowekwa katika baadhi ya halmashauri hayaendani na hali halisi
na kutolea mfano wa halmashauri ya Busega kuwa na lengo la kukusanya
milioni 30 wakati inadai milioni 343 kutoka kwa wadaiwa wa kodi ya
pango la ardhi.
Kaimu Mkuu wa
mkoa wa Simiyu ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga
alimuhakikishia Naibu Waziri wa Ardhi, halmashauri za mkoa huo zitaanza
kuwafuatilia wadaiwa wote wa kodi ya pango la ardhi sambamba na
kuhakikisha viwanja vinaingizwa katika mfumo na kuwahamaisha wananchi
kuchukua hati za ardhi ili kuongeza kasi ya makusanyo ya kodi ya ardhi.
Kiswaga
alipongeza maboresho mbalimbali yanayofanywa na wizara ya ardhi katika
masuala ya utoaji huduma hizo na kutolea mfano uanzishwaji ofisi za
ardhi za mikoa kuwa ni moja ya mambo yatakayoleta ufanisi katika sekta
ya ardhi.
No comments :
Post a Comment