Wednesday, April 1, 2020

JAFO ARIDHISHWA NA UJENZI WA HOSPITALI YA UHURU DODOMA,ATOA MAAGIZO UJENZI WA OFISI YA DC



Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akiwasili katika eneo la ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi huo leo jijini Dodoma.
Mafundi kutoka Suma JKT wakiendelea na ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akiendelea kukagua ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kujionea maendeleo ya ujenzi huo leo jijini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua na kujionea ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma alipofanya ziara leo jijini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi huo leo jijini Dodoma.
Kaimu katibu tawala mkoa wa Dodoma Mhandisi Happiness Mgalula akitoa maelezo kwa Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo (hayupo pichani) alipofanya ziara ya  kukagua na kujionea ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma alipofanya ziara leo jijini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa maelekezo ya Mhe Rais Dk John Magufuli katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma mara baada ya kufanya ziara huku akiridhishwa na ujenzi huo.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa maelekezo ya Mhe Rais Dk John Magufuli katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo akimsikiliza Mhandisi kutoka Suma JKT Bw.Omari Kabalagu anayesimamia ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa maelekezo ya Mhe Rais Dk John Magufuli katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma mara baada ya kufanya ziara huku akiridhishwa na ujenzi huo.
…………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Uhuru inayojengwa katika
halmashauli ya wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma  katika ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Uhuru na ujenzi wa jingo la mkuu wa wilaya ya Dodoma.
“Chachu ya kasi ya ujenzi huu imeongezwa na nguvu kazi ya watu  200 iliyo ongezwa na kukamilisha idadi ya watu 300 ili kuendana na muda uliyopangwa wa kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo”, amesema Mhe. Jafo.
Pia Mhe. Jafo ametoa rai kwa Mwenyekiti  wa Kamati ya Ujenzi huo kuandaa mpango kazi utakao leta mabadiliko ndani ya wiki mbili ili mtu yeyeto atakaye fika katika ujenzi huo aweze kukuta kuna mabadiliko makubwa katika ujenzi.
Aidha Mhe. Jafo amemtaka Mkurugenzi wa wilaya ya Chamwino  kufikisha vifaa vya ujenzi kwa wakati ili kutatua changamoto ya vifaa kutofika kwa wakati saiti jambo ambalo linaweza kufanya ujenzi kusikamilike kwa muda uliyopangwa.
Kwa upande wa Mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino Bw.Athumani Masasi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maono yake ya kujenga hospitali hiyo kubwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watanzania na wananchi wa nchi za jirani.
Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino inajengwa baada ya Rais Magufuli kuelekeza kufanya hivyo katika sherehe za Uhuru mwaka 2018 na kuelekeza fedha zilizokuwa zitumike kwenye maadhimisho ya sherehe hizo kujenga Hospitali hiyo mkoani Dodoma.
Awali Waziri Jafo alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma ambapo amesema kuwa hajaridhishwa na ujenzi huo kutokana na nguvu kazi kuwa ndogo.
”RC wa Mkoa kiukweli bado  kasi ya ujenzi huo hainiridhishi kutokana na idadi ndogo ya nguvu kazi kutoka  JKT hivyo nawaomba muongeze kasi ili kufikia Mei 7,mwaka huu kama mlivyosema mkabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Wilaya”amesema Jafo

No comments :

Post a Comment