…………………………………………………………………………………..
Inaripotiwa, kuwa Chicago peke yake, asilimia 70 ya waliokuga kwa Corona ni Wamarekani weusi.
Kwamba zaidi ya nusu ya
waliothibitishwa kuwa na virusi Chicago ni Afro- Americans. Hata kama
idadi ya weusi wote kwa ...
asilimia Chicago ni asilimia 30 tu.
Hali ni hivyo hivyo kwenye majimbo mengi ya Marekani. Loussiana, moja ya majimbo yalioathirika vibaya yana hali hiyo hiyo.
Kwanini?
Kuna kuna pengo kubwa kati ya
masikini na matajiri. Marekani yenye mfumo wa kibepari haijali sana kuwa
na mifumo ya afya ya kijamii.
Obama Care ilitupiliwa mbali na Trump. Marekani kuna wenye kuamini kuwa mifumo hiyo yenye kujali ustawi wa wengi ni ya Kijamaa.
Ona ilivyo sasa. Weusi wengi
hawana kazi. Ni vibarua tu. Ni wagonjwa kuanzia kifua kikuu mpaka
kisukari. Hawana bima. Wenzao weupe waliwahi mapema kupima virusi. Weusi
hawakuwa na fursa hiyo. Hawana fedha.
Wengi wamekwenda vibaruani wakiwa na virusi au wagonjwa. Wameambukiza wengine na wameambukizana nyumbani.
Kauli za kuwataka watu wabaki
majumbani hazikuwa na maana kwao, wangekula nini? Kazini ili waajiri
wawape ruhusa ya kubaki nyumbani kwa vile ni wagonjwa, basi, walihitaji
kuonyesha cheti kama wamepima na wameonekana na virusi.
Masikini Wamarekani weusi wale,
hawakuw na hela za kupimia. Catch- 22. Aliandika mwandishi Joseph
Heller. Ameelezea hali kama hii.
Naam, tuliambiwa zamani sana, kuwa Ubepari ni unyama.
Maggid
Dar Es Salaam.
No comments :
Post a Comment