Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa maelekezo
alipotembelea eneo la bahari kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na
changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na
White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta
unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (mwenye kofia) akiwa
ameambatana na wataalamu wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi
na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akiwa katika ufukwe alipofika
kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira
kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es
Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na
hivyo maji kujaa.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.
Samuel Gwamaka akimpa maelekezo Afisa Sheria na Utawala kutoka hoteli ya
Wellworth, Saimon Nguka kuhusu kufanya Tathmni ya Athari za Mazingira
(EIA) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu katika eneo hilo jijini
Dar es Salaam alipofika kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na
changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na
White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta
unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.
Samuel Gwamaka apofika eneo la ufukwe wa bahari jijini Dar es Salaam
wakati alipofika kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira
kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es
Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na
hivyo maji kujaa.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amewataka wataalamu
wa mazingira kufanya tathmini ya mazingira katika maeneo ya
bahari
kupata dawa ya madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Zungu alitoa kauli hiyo alipofanya
ziara katika eneo la bahari lenye mgogoro kati ya Motison wanaomiliki
hoteli ya Whitesand wakituhumiwa na wamiliki wa hoteli ya Wellworth
Kunduchi kwa kujenga ukuta baharini hatua iliyosababisha maji kujaa
hotelini kwao.
Akizungumza katika eneo hilo akiwa
ameambatana na watendaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) waziri huyo aliwataka kuwa wavumilivu kusubiriwa
wataalamu wa sayansi ya bahari wafanyie kazi na kutoa majibu wiki ijayo.
Hata hivyo Waziri Zungu aliwataka
wananchi kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwani ndio sababu kubwa ya
maji ya bahari kujaa isivyo kawaida na kuingia katika maeneo yao.
“Leo tunatazama mgogoro wa watu
wawili kesho tutakuwa na wa watu watano au sita, tupeni muda nimekuja
hapa na mkurugenzi wa NEMC na wataalamu wake kutazama na dawa ya
changamoto tunayo kwa hiyo wiki ijayo tutawaita na tutawaambia
tulichofanya kuhakikusha kila mtu ana amani ndiyo kazi ya Serikali,”
alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
NEMC Dkt. Samuel Gwamaka aliwataka wawekezaji wote kufanya tathmni ya
athari za mazingira (EIA) ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima,
Alisema kuwa binadamu tunaishi kwa
kutegemeana kwenye mazingira na ndiyo maana NEMC haitoi cheti hadi
ifanyike tathmnini hiyo kubaini madshara yanayoweza kutokea kwa wananchi
kupitia uwekezaji unaofanyika.
“Natoa rai kwa wawekezaji wote
wawe wa viwanda ama htoeli katika fukwe zetu kufanya tathmni na kupitia
tathmini hiyo tutapata maoni kutoka kwa watu wanaokuzunguka kujua je
uwekezaji wako unawaathiri vipi na kama kuna athari ndogo tunajua namna
ya kuzitatua ili kuepusha migioogoro,” alisisitiza.
Akitoa maoni yake kuhusu
changamoto hizo Mtaalamu wa Sayansi ya Bahari Rose Mtui alisema kuwa
suluhisho ni kuotesha mikoko ambayo inalunda fukwe zikibomoke kutokana
na mmomonyoko wa udongo.
Aliongeza kuwa uchimbaji mchanga
holela katika kingo za miti na uvuvi haramu unachangaia changamoto za
kimazingira katika fukwe za bahari kwani unaharibu matumbawe ambayo
yakiharibika mawimbi ya bahari higonga moja kwa moja na kwa kasi fukwe
na hivyo maji kujaa kupita kiasi.
No comments :
Post a Comment