Mkurugenzi
mkuu wa Shirila la Fedha Duniani IMF Bibi Kristalina Georgieva amesema
kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, uchumi wa dunia kwa mwaka huu
unakadiriwa kushuhudia mporomoko mkubwa zaidi tangu miaka ya 30 ya karne
iliyopita.
Amesema
mlipuko wa virusi vya Corona ni msukosuko pekee, ambao unavuruga kwa
kasi na kwa kina utaratibu wa kijamii na kiuchumi kote duniani.
Katika miezi mitatu iliyopita, IMF ilikadiria kuwa mapato ya watu katika nchi wanachama zaidi ya 160 yataongezeka mwaka huu, lakini kwa sasa shirika lake limekadiria kuwa mapato hayo katika nchi zaidi ya 170 yatapungua mwaka huu.
Shirika hilo litatoa ripoti mpya kuhusu makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia wiki ijayo.

Ameongeza
kuwa kama mlipuko wa virusi vya Corona utadhibitiwa katika nusu ya pili
ya mwaka huu, na nchi zote zitarejesha shughuli za kiuchumi, uchumi wa
dunia utafufuka kwenye baadhi ya sehemu, lakini bado utakabiliwa na
sintofahamu kubwa.
No comments :
Post a Comment