Jimbo
la New York nchini Marekanai sasa lina visa vingi vya virusi vya corona
zaidi ya taifa lolote duniani , kulingana na takwimu mpya.
Serikali
imethibitisha kwamba idadi ya visa vya ugonjwa huo imeongezeka kutoka
10,000 siku ya Alhamisi hadi 159, 937 na kuiweka mbele ya Uhispania ilio
na visa 153,000 na Itali ilio na visa 143,000.
China
ambapo virusi hivyo vilianza mwaka uliopita iliripoti visa 82,000.
Marekani yote imerekodi visa 462,000 na takriban vifo 16,500.
Kote duniani kuna takriban visa milioni 1.6 na vifo 95,000.
Huku
Jimbo la New York likiongoza ulimwengu katika visa vya maambukizi ,
takriban watu 7000 wamefariki katika mji huo , ikiwa nyuma ya Uhispania
ilio na vifo 15,500 na Itali ilio na 18,000 ikiwa ni mara mbili ya vifo
vya China 3,300.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
No comments :
Post a Comment