Afisa wa Maji Bonde la Kati, William Mabula, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukagua athari za mafuriko kufuatia kujaa kwa maziwa ya Kindai, Munang na Singidani mkoani hapa jana.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala, akionesha athari za mafuriko hayo.
Muonekano wa Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Kati mkoani Singida.
Na Waandishi Wetu, Singida
KUFUATIA
mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha Bodi ya Maji Bonde la Kati
imewataka wamiliki wote wa mabwawa yote ya tope sumu kuhakikisha
wanadhibiti maji kuweza kusambaa kwenye mazingira kwa kuweka miundombinu
thabiti, ikiwemo kuboresha miundombinu iliyopo ili kutoruhusu maji
yenye sumu kufika kwa wananchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani hapa jana, mara baada ya kukagua athari
za mafuriko kufuatia kujaa kwa maziwa ya Kindai, Munang na Singidani,
Afisa wa Maji Bonde la Kati, William Mabula, alisema kwa yeyote
atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua kali.
“Wamiliki
wote wa mabwawa ya maji na yote ya tope sumu hakikisheni mnadhibiti
maji kuweza kusambaa kwenye mazingira kwa kuweka miundombinu thabiti
ili kutoruhusu maji yenye sumu kufika kwa wananchi,” alisema Mabula.
Aidha,
Mabula aliwataka wananchi wote wakiwemo wamiliki wa mabwawa ya maji na
mabwawa ya tope sumu kuchukua tahadhari kwa kuzingatia matangazo ya
utabiri wa hali ya hewa yanayoendelea kutolewa kuhusu mvua hizo
zinazoendelea kunyesha kwa kasi kote nchini.
Alisema
mvua hizo zinaweza kusababisha mabwawa kujaa maji zaidi ya uwezo wake
hivyo kutishia usalama wa wananchi, mali zao na mazingira kwa ujumla.
Kujaa kwa mabwawa hayo kunaweza kusababisha yakapasuka au kutiririsha
maji katika mikondo isiyo rasmi na madhara yake yanaweza kuleta mafuriko
katika vijiji, barabara, madaraja, na kuharibu miundombinu mingine.
Pamoja
na mambo mengine, Afisa huyo aliwashauri kwa kuwakumbusha wamiliki wote
wa mabwawa ya maji kusafisha utoro wa maji, kuimarisha tuta la bwawa
kwa kuondoa miti yenye mizizi, na vichuguu juu ya tuta, kuziba matoleo
yote yanayotumika kutolea maji wakati wa kiangazi na kutunza uoto wa
asili ili kudhibiti uingizaji wa mchanga kwenye bwawa, ikiwemo kupanda
mimea au miti rafiki ya kupunguza kasi ya kuingiza michanga kwenye
bwawa.
Aidha
aliwatahadharisha wananchi wote wanaoishi chini ya utoro wa maji wa
mabwawa na wale wanaoishi kuzunguka migodi kuchukua tahadhari ya kupata
mafuriko kutokana na kipindi hiki mabwawa mengi kujaa maji zaidi ya
uwezo wake.
“Lakini
kwa mujibu wa sheria nawakumbusha wamiliki wote wa mabwawa kuwasilisha
mipango ya usalama wa mabwawa na mafuriko kwa Mkurugenzi wa Rasilimali
za Maji ili kukabili dharula itakayoweza kutokea kutokana na mvua za
masika zinazoendelea kunyesha,” alisema Mabula
No comments :
Post a Comment