Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama
mkoa wa Arusha kwenye Soko la Samunge kuhakikisha Serikali inaweka
miundombinu sawa kwa haraka ili wafanyabiashara kazi zao picha zote na
Ahmed Mahmoud Arusha
Majadiliano ya viongozi wa Serikali mkoa wa Arusha kwenye soko la Samunge jijini Arusha wakati ukarabati wa miundombinu ukiendelea leo |
Biashara zikiendelea mama akiwa na sufuria kichwani akipita katika ya eneo la Soko la Samunge kuendelea na kazi za Ujenzi wa taifa |
Wafanyabiashara wakisubiria kuhakiki maeneo yao kabla ya ujenzi kuanza |
Biashara zinaendelea huku wafanyabiashara wakingojea kupangiwa maeneo na Serikali kupitia Uongozi wao kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha. |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali mkoani hapa
imehamia kwenye soko la Samunge lililoungua mwishoni mwa wiki kwa lengo
la kuhakikisha kila mfanyabiasha anapata eneo lake pamoja na kuona
uwekaji sawa wa miundombinu na ugawaji wa maeneo ndani ya soko hilo.
Akiongea kwenye
hadhara hiyo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alieambatana na kamati
ya Ulinzi na Usalama mkoa tokea Asubuhi ya Leo amesema kuwa atahakikisha
kila mfanyabiashara aliekuwepo kwenye soko hilo anapata eneo la
kufanyabiashara.
Alisema kuwa wapo
watu wanaotaka kutumia nafasi hiyo kujipenyeza amewataka kukaambali
kwani Serikali haitasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria pamoja na
wale wanaodhani huu Sasa ni wakati wa kufanya mzaha waache Mara moja
kwani hayo ni maisha ya watu.
Amewatoa hofu
wafanyabiashara hao na kuahidi Serikali kuwepo eneo hilo kwa siku nzima
ya leo kuona kila alieunguliwa anapata eneo lake ili aanze ujenzi Mara
moja ikiwemo na kufanyabiashara.
Amebainisha kuwa
Serikali itaendelea kuwepo kwenye eneo hilo na kusaidia kuona
wafanyabiashara hao wakianza shughuli za kujipatia kipato kwani
wanategemewa na kama tutachelewesha kumaliza familia zao zatakufa njaa
ndio maana tupo hapa Leo nzima.
Kwa Upande wake Kaimu
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Joseph Massawe ameendelea kuitaka
Serikali kuhakikisha inamaliza kuweka miundombinu kwa haraka ili
wafanyabiashara hao waanze kazi Mara moja
Nae Kamanda wa Kikosi
Cha Zimamoto alisema kuwa miundombinu hiyo ya barabara itaanzia kusini
na kaskazini na upande mashariki na magharibu kutakuwa na barabara
ambayo itasaidia pindi litakapotokea tukio kama hilo kuwe na njia ya
kupitika kuweza kuzima na kuokoa Mali kwa haraka tofauti na kipindi
kilichopotia.
Awali kaimu kamanda
wa Polisi mkoani hapa Koka Moita aliwatoa hofu wafanyabiashara hao na
kuwaambia jeshi hilo litashuhulika na yeyote ambaye atabainika kuleta
uvunjifu wa Amani katika eneo hilo na wataendelea kufuata maagizo ya
mkuu wa mkoa hadi kuona kila moja anafanya kazi zake kwa usalama.
No comments :
Post a Comment