Mkurugenzi
Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF) Joseph Manirakiza kulia
akizungumza na waandishi wa habari juu ya wiki ya ubunifu itakayoanza
Machi 8 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu
Kiongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo wa Uingereza (DFID) Natalie
Smith na kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dr. Amos
Nungu.
Mtaalamu
wa Mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF)'Hannah
Mwandoloma akiwakaribisha wadau wa Maendeleo katika mkutano wa
waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Ubunifu itakayoanza Machi 8 hadi 13
jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Kiongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo wa Uingereza (DFID) Natalie
Smith katikati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya wiki ya
ubunifu itakayoanza Machi 8 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katikati ni na kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia
Dr. Amos Nungu na kulia niMkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Watu
(HDIF) Joseph Manirakiza.
Mtaalamu
wa Mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF)'Hannah
Mwandoloma akiwakaribisha wadau wa Maendeleo katika mkutano wa
waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Ubunifu itakayoanza Machi 8 hadi 13
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari katika mkutano huo
ZAIDI
ya wabunifu 700 nchini wamepata ajira za moja kwa moja kutokana na
bunifu mbalimbali walizozifanya kwa maendeleo huku wengine 14,000
wakipata ajira za muda.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Darves salaam leo Machi 5, 2020
Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu
amesema serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF)
kwa ufadhili na Serikali ya Uingereza wameandaa wiki ya ubunifu ili
kuona bunifu mbalimbali zenye kuchagiza maendeleo.
Amesema
maonesho hayo ambayo ni ya awamu ya sita kufanyika hapa nchini
yatawakutanisha wabunifu na wadau zaidi ya 6000 ambayo yatafanyika
katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Arusha na
Zanzibar na yanaenda kwa kauli mbiu ya 'Buni kwa tija'.
Amesema
maonesho hayo yataanza Machi 8 mwaka huu lakini yatafunguliwa Machi 9
na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha.
"Serikali
imekuwa ikihakikisha mfumo wa ubunifu unahusisha wabunifu, wadau wa
maendeleo na jamii hivyo, tunajivunia matokeo chanya yanayopatikana
kupitia ubunifu kwa kipindi cha zaidi ya miaka saba tokea mwa 2011.
Amesema
kwa kuanzia waliwatengeneza wabunifu 110 kwa kupitia atamizi mbalimbali
ambapo zaidi ya Sh bilioni 1.9 zilitoewa na kusababisha mtazamo wa
sekta nyingi ikiwemo za serikali kutumia ubunifu katika shughuli zao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkazi wa HDIF, Joseph Manirakiza amesema
walianza kuandaa wiki ya ubunifu mwaka 2015 kwa kuangalia sekta za maji,
afya, elimu na usafi na kwamba kwa kuanzia hapo wabunifu mbalimbali
wamekuwa wakiunganishwa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kuwapatia
fedha za kuendeleza bunifu zao.
Ameongeza
kuwa, kutokana na kukua kwa uelewa kuhusu ubunifu watu wengi
wameendelea kujitokeza kufanya bunifu kwa malengo ya kutatua changamoto
mbali mbali kwenye jamii zikiwemo za kiuchuni na kuongeza ushirikiano
baina ya sekta binafsi na serikali.
''Wiki
ya Ubunifu ilianza kwa washindi wa masuala ya ubunifu katika sekta hizo
kuonesha bunifu zao kwa wadau na baadae kupewa fedha za ujiendeleza
lakini baadae tuliamua kuwakutanisha wabunifu na wadau wa maendeleo ili
kujadiliana namna ya kuendeleza kazi zao hivyo, tunaendelea kupanua
huduma tulianza na Dar es Salaam na sasa tunafikia mikoa sita na malengo
ni kufikia mikoa yote nchini,'' alisisitiza Manirakiza.
Naye,
Kaimu Kiongozi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kimataifa wa Uingereza (DFID)
Natalie Smith amesema wiki ya ubunifu ambayo inafanyika kwa mara ya sita
sasa imesaidia ukuaji wa sekta hya ubunifu nchini Tanzania kuongeza
ukuaji wa maendeleo na ongezeko la wafadhili.
Amesema
serikali ya Tanzania pia imeongeza uwekezaji katika sekta ya ubunifu
kwa kuandaa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
(MAKISATU 2020) yatakayofanyika mkoani Dodoma.
Mwaka
huu HDIF CISTECH imeandaa wiki hiyo ya ubunifu kwa kushirikina na wadau
mbali mbali wakiwemo UNDP, UNICEF, UN, WOMEN, UNCDF CLOUDS MEDIA,
SEGAL FAMILY FOUNDATION, EXIM BANK na Ubalozi wa Netherland.
No comments :
Post a Comment