*****************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amekabidhi matreka 19 yenye thamani ya sh. bilioni 1.520
yaliyolewa kwa mkopo na Benki za NMB na CRDB kwa ajili ya wakulima wa
mkonge wanaounda Vyama vya Msingi (AMCOS) vinne vya kilimo cha mkonge.
Ameyasema hayo
leo(Alhamisi, Machi 5, 2020) baada ya kutembelea eneo eneo la shamba la
mkonge la wakulima wadogo Mwelya Sisal Estate na kujionea shughuli za za
usindikaji mkonge na kukabidhi matrekta kwa wakulima.
Benki ya NMB
imetoa matrekta 11 na matera 22 yenye thamani ya sh. bilioni moja na
CRDB imetoa matrekta manane na majembe yake yenye thamani y ash.
milioni 520.
Waziri Mkuu
amesema zao la katani ni miongoni mwa mazao saba ya biashara nchini,
hivyo amewahamasisha wananchi kulima zao hilo kwa wingi. “Maafisa kilimo
hakikisheni mnawasaidia wakulima kuanzia hatua za awali za utayarishaji
shama hadi mavuno hadi utafutaji wa masoko.”
Amesema lazima
zao hilo liuzwe kwa mfumo wa ushirika, wanatambua kuna wakulima wakubwa,
wadogo na wa kati wote wanatakiwa waratibiwe vizuri ili wanaohitaji
waende kununua kwa mfumo huo na namna ya kuuza iwe ya ushindani.
Pia, Waziri Mkuu
amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima zao la mkonge waratibu na
kuwatambua wakulima wote katika maeneo yao wawasajili na kuwaunganisha
katika ushirika ambao utasaidia katika kuwapa elimu na namna bora
kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kupata pembejeo na zana za kilimo.
Kadhalika, Waziri
Mkuu amezipongeza benki kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu
ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwasaidia
wakulima kwa kuwakopesha matrekta ambayo yatarahisha shughuli za kilimo
cha zao hilo la mkonge.
Hata hivyo,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa AMCOS wahakikishe wanatoa
taarifa za mapato na matumizi kwa wanachama wao na pia hata wanapokopa
mikopo wawajulishe wanachama na wasitumie vibaya madaraka yao na kula
mali za ushirika.
Amesema vyama
vingi vya ushirika vimekufa kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa
waaminifu wanaoshiriki katika kufuja mali za ushirika. “Serikali
itawafikisha mahakamani viongozi wote wa ushirika wasiokuwa waaminifu.”
“Viongozi kama
mnafikiria kwenda kwenye ushirika kwa ajili ya kuondoa umasikini
usichukue fomu na kama upo madarakani andika barua ya kujiuzulu leo.
Tutafanya uchunguzi na tukikubaini tutakupeleka mahakamani, hatuna mzaha
na fedha za wananchi. Tumedhamiria kurugudisha ushirika wenye tija kwa
wananchi.”
Kwa upande
wake,Naibu Waziri wa Kilimo Omar Mgumba amesema awali mashamba hayo
manane ya mkonge yalikuwa yanamilikiwa na Serikali na kisha
waliyabinafsisha matatu na matano yakabakia chini ya Bodi ya Mkonge.
Naibu Waziri huyo
amesema Bodi ya Mkonge waliwapa wakulima wadogo wayaendeleze lakini kwa
kipindi chote cha miaka 14 kuanzia 2004 hadi 2018 walikuwa wanalima na
mapato yote yalikuwa yakwenda kwa muwekezaji kutokana na mfumo
uliokuwepo.
Naye,Mweyekiti wa
Wenyeviti wa AMCOS za zao la mkonge mkoani Tanga za mashamba ya Magoma,
Magunga, Mwelya, Hale na Ngombezi, Bw. AmGreyson Nnyari amesema AMCOS
zao zina jumla ya wanachama 1,081.
Amesema kilimo
cha mkonge kwa kuwashirikisha wakulima wadogo kilianza 1999 katika
shamba la Mwelya na kuenea kwenye mashamba yay a Magoma, Magunga,
Ngombezi na Hale ilipofika 2002 na muasisi wa mfumo huo ilikuwa Kampuni
ya Katani Limited.
“Baada ya kampuni
ya Katani Limited kuendesha mfumo huo kwa miaka 14 malalamiko mengi
yalijitokeza kutoka kwa wakulima na kuonesha kuwa mfumo huo haukuwa
rafiki kwa sababu mkulima alikuwa analipwa kiasi kidogo na fedha na kwa
wakati anaotaka yeye licha ya mkulima kusimamia shughuli zote za shamba
kuanzia hatua na uuandaji, upandaji, uvunaji na usafirishaji wa mkonge
hadi kiwandani.”
Amesema baada ya
malalamiko hayo ya wakulima kufikishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bw.
Martine Shigela aliunda kikosi kazi ambacho kilijumuisha Bodi ya Mkonge
na Halmashauri ya wilaya ya Korogwe ili kubaini ukweli wa madai ya
wakulima.
Bw. Nnyari
amesema baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi hicho ni
pamoja na kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa kilimo hicho kwa wakulima
wadogo na kuagiza Mkaguzi Mkuu wa Heshabu za Serikali kufanya uhakiki wa
kubaini uhalali wa madeni yote ambayo kampuni ya Katani inadaiwa na
ambayo inawadai wakulima.
“Baada ya
uchunguzi huo Serikali ilibaini kwamba Kampuni ya Katani Limited
iliwapunja wakulima kuanzia 2008 hadi 2018 jumla ya sh. bilioni 29.4
ambazo ni pamoja na fedha za SACCOS na AMCOS. Aidha wakulima nao
walikuwa wanadaiwa kiasi cha sh. bilioni 2.8.”
Amesema Desemba
2018 Serikali ilifanya mabadiliko kwa kuiondoa Kampuni ya Katani Limited
katika shughuli za wakulima na kuipa AMCOS kazi ya kusimamia shughuli
zote kuanzia utayarishaji wa mashamba, uvunaji na uuzwaji ambao kwa sasa
unafanyika kwa kupitia minada na mnunuzi anapatikana kwa njia ya
ushindani tofauti na awali ambapo kampuni ya katani ilikuwa mnunuzi
pekee.
Mwenyekiti huyo
ametaja mafanikio yaliyopatikana baada ya AMCOS kupewa uendeshaji wa
mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato ya mkulima kutoka
sh. 206,000 kwa tani moja hadi kufikia sh. milioni 1.450.
No comments :
Post a Comment