Monday, March 9, 2020

WANAWAKE WAMETAKIWA KUPAMBANA NA MAJANGILI WA WANYAMAPORI.




Watumishi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA )
Mkoa wa Morogoro wakiwa katika maandamano,katika siku ya Wanawake Duniani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. 
*************************
NA FARIDA SAIDY MOROGORO
Wakati Dunia inaadhimisha siku ya Wanawake Duniani Wanawake Nchini  wametakiwa  kuwa
mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Majangili ili kulinda Nyala za Serikali hususani Wanyamapori.

Wito huo umetolewa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani,Manispaa ya Morogoro  na Bi Cassia Mayombo kutoka kitengo cha Utawala Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania(TAWA ) alikupokuwa anaongea na Fullshangwe Blog,ambapo amesema kuwa wao kama TAWA wanatambua mchango wa Wanawake katika kupambana na Majangili.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mwandamizi Mahusiano kwa Umma kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bwana Twah Twahibu amesema kuwa Askari  Wanawake wa Wanyamapori(JESHI USU) wapo vizuri katika kupambana na majangili wawapo porini hivyo amewataka kuongeza kasi zaidi katika kazi yao.

Aidha amesema kuwa Mamlaka hiyo ipo katika mchakato wa kufungua mabucha na mashamba ya kufugia Wanyamapori,hivyo wamewataka wadau mbalimbali kujitokeza kuomba nafasi hizo zitakazokuza kipato
chao na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine amewataka Wananchi hususani wa Mkoa wa Morogoro kutumia njia mbadala ya kuwafukuza Tembo wanaoingia katika mashamba yao kwakuweka mizinga ya nyuki jambo litakalowasaidia kuepukana na wanyama hao kipindi Mamlaka ikiwa inaagalia namna ya kukabiliana na Wanyama hao.

No comments :

Post a Comment