Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri (katikati) na viongozi wa Wilaya ya Kaliua wakiwa
wameshika mfano wa hundi ya milioni 345 iliyotolewa kwa vukundi 57
ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani iliyotolewa jana siku
ya wanawake duniani.
***********************
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua
imekabidhi mkopo wa shilingi milioni 345 kwa vikundi 57 ikiwa ni sehemu
ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani katika mwaka wa fedha
unaoendelea.
Taarifa hiyo imetolewa leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima wakati wa
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yalifanyika jana
Wilayani humo.
Alisema kati ya fedha hizo vikundi
28 vya wanawake vimepokea milioni 184, vikundi 19 vya vijana
vimekopeshwa 133.5 na vikundi 10 vya walemavu vimekpeshwa milioni 27.
Alisema fedha hizo ni sehemu ya
utekelezaji ilani yaChama cha Mapinduzi iliyoagiza kutenga asilimia 10
kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa vikundi hivyo.
Dkt Pima alisema tangu nwaka 2015
hadi desemba 2019 , Kaliua ilikuwa imeshatoa jumla ya mikopo ya shilingi
milioni 839.7 kwa vikundi 209.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema hadi
hivi jumla ya shilingi milioni 591.9 bado haijarejeshwa kitendo ambacho
kimewafanya waandikie notisi ya 90 ili warejeshe.
Dkt. Pima alisema baada ya hapo wadaiwa sugu wote watachukuliwa hatua za kisheria.
Akikabidhi hundi kwa vikundi ,
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amevitaka vikundi ambavyo bado
havijaresha mikopo waliopatiwa kurejesha ili iweze kuwasadia wengine.
Aliipongeza Halmashauri ya Wilaya
ya Kaliua na kuzitaka Halmashauri nyingine za Mkoa wa Tabora kuhakikisha
wanatenga asilimia 10 za mapato yake ya ndani kwa ajili ya kupeleka
katika vikundi kama ilivyoelekezwa.
Mwanri alisema kuwa ni vema
Halmashauri zikahakikisha zinatoa fedha ambazo zitavisaidia vikundi
kupata matokeo mazuri na kuwapatia maendeleo.
No comments :
Post a Comment