Mkuu wa Taasisi wa Ustawi wa Jamii
Dkt.Joyce Nyoni akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa tiba katika
hospitali ya Palestina-Sinza katika maadhimisho ya siku ya wanawake
Duniani
Baadhi ya wanawake wa Taasisi ya
Ustawi Ustawi wa Jamii wakiwa katika Hospitali ya Palestina wakati
walipopeleka msaada wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.
Sehemu ya Vifaa Tiba vilivyotolewa katika Hospitali ya Palestina na Wafanyakazi Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
***************************
Wafanyakazi Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii imetoa msaada
wa vifaa tiba mbalimbali katika hospitali ya Palestina-Sinza ikiwa ni
kuadhimisha siku ya
wanawake duniani kwa kutambua kama wanawake
wanawajibu wa kuunga mkono serikali katika sekta ya afya.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi vifaa tiba hivyo Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce
Nyoni amesema kuwa vifaa tiba hivyo vimetokana na mchango wa wananwake
wa Taasisi hiyo kwa kuamini wanaweza bila kuwezeshwa.
Amesema kuwa vifaa tiba walivyotoa wanaamini kuwa vitasaidia katika mahitaji ya Hospitali kwa kuhudumia wagonjwa wanaofika hapo.
“Sisi wanawake tunaweza ndio maana
baada ya kutambua siku ya wanawake duniani inakuja tukajichanga kutoka
mifukoni mwetu ili kuweza kufikia azima ya kununua vifaa tiba na
kufikisha katika hospitali ili ndugu,jamaa na watoto wanaofika kuweza
kutumia”amesema Dkt.Nyoni.
Nae Mratibu wa Huduma Tiba wa
Hospitali ya Palestina-Sinza Dkt.Nchang’wa Nhumba amewapongeza wanawake
wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kutambua Palestina wanahitaji msaada
kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika katika
hospitali hiyo.
Dkt.Nhumba amesema kuwa Wanawake
wa Ustawi wa Jamii waendelee kuwa na moyo huo hata wakati mwingine
waweze kwenda kusaidia na kuongeza kuwa wanawake wa Taasisi zingine
kuiga mfano huo.
No comments :
Post a Comment