Monday, March 2, 2020

WAANDISHI WASHAURIWA KUBOBEA KWENYE ENEO MOJA ILI KUANDIKA HABARI KWA UMAHIRI



 Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi wa BoT jijini Arusha Machi 2, 2020.
  Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi wa BoT jijini Arusha Machi 2, 2020.
 Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina akitoa maelezo ya awali kuhusiana na semina hiyo
 Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina (katikati) akitoa maelezo ya awali kuhusiana na semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa BoT tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akitoa mada kuhusu mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia na matarajio kwa mwaka 2020.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akitoa mada kuhusu mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia na matarajio kwa mwaka 2020.

 Dkt. Deogratius Assey, Meneja Udhibiti Ustahimilivu wa Sekta ya Fedha na Majanga




NA Khalfan Said, Arusha
MKURURGENZI wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Arusha, Bw. Charles Yamo amewashauri waandishi wa habari kuchagua eneo la kubobea katika sekta fulani ili kuandika kwa umahiri habari husika. Bw. Yamo ameyasema hayo leo Machi 2, 2020 wakati akifungua semina ya waandishi wa
habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi wa BoT jijini Arusha.
“Ni lazima kubobea katika sekta fulani kiuandishi, huwezi kuwa mwandishi
unayeandika kila kitu, kwahiyo lazima kuwepo na specialization,
Alisema kama ukitaka kuwa mwandishi wa habari za kilimo hakikisha unatumia nafasi kubwa ya muda wako kujifunza sekta hiyo inavyofanya kazi ili iwe rahisi kwako
kuandika makala kuhusu sekta hiyo.
“Huwezi kuwa mwandishi wa habari mzuri kama wewe leo unakuwa kwenye siasa, kesho kwenye kilimo keshokutwa michezo, mtondogoo uchumi unagusa gusa kila eneo…ukitaka kubobea kwenye eneo fulani…lazima uchague, usipofanya hivyo uandishi wako
utatia mashaka na utamuacha msomaji anaelea….” Alisema.
Pia Bw. Yamo alishauri kuwa ni muhimu kwa waandishi wa habari kujiendeleza kielimu,
kwani dunia inabadilika kwa kasi sana hasa katika teknolojia ya habari na
mawasiliano yaani (TEHAMA).
“Usipobadilika unaweza kujikuta uwepo wako katika taasisi yako usiwe na tija au kazi yako isifikie malengo kama ambavyo ungependa…. hivyo ni muhimu kwa sasa kwa mwandishi wa habari kuwa na uwezo wa kutayarisha habari na kuwafikia wananachi kwa njia mbalimbali na rahisi.” Alisisitiza Bw. Yamo.
Aidha Mkurugenzi huyo aliwaasa waandishi w ahabari kuwa wazalendo kwa taifa lao na kujiepusha na kutoa taarifa zisizo na tija kwa taifa.
Akizungumza mwanzoni mwa semina hiyo, Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina alisema, washiriki wa semina hiyo wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya televisheni, radio, magazeti na mitandao ya kijamii na kwamba semina hiyo itadumu kwa siku tano ambapo wataalamu wa BoT watatoa elimu kuhusu shughuli za BoT.

No comments :

Post a Comment