Na.Alex Sonna,Dodoma
Rai hiyo
imetolewa leo Machi,2,2020 jijini Dodoma na Waziri wa nchi,Ofisi ya
Rais ,Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteini Mstaafu
George Mkuchika wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa mapambano
dhidi ya rushwa kwa kuwatumia
vijana wa skauti nchini.
Kaptein Mkuchika
akizungumza kwa niaba ya mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,makamu wa Rais
Samia Suluhu,amesema rushwa inadhoofisha haki hivyo ni jukumu la kila
mmoja katika mapambano hayo.
“Mapambano
dhidi ya rushwa ni jukumu letu sote tushiriki mapambano dhidi ya rushwa
,ninyi vijana wa skauti mkawe mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwa
umma”amesema.
Kwa upande wake
,Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi ameitaka jamii
kukitumia vyema Kiswahili fasaha katika kutoa elimu juu ya madhara ya
rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.
Mskauti mkuu
Tanzania Mwamtumu Mahiza amesema zaidi ya wanafunzi milioni 10 na laki
6 wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wameandaliwa kusambaza
elimu ya rushwa ambapo matarajio ni kufikia watu milioni 40 kupata
elimu hiyo.
Kaimu mkurugenzi
mkuu wa TAKUKURU nchini Brigedia Jen John Mbungo amesema Mpango wa
Uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa mapambano dhidi ya rushwa kwa kutumia
vijana wa skauti nchini utasaidia kuongeza vijana maaskari wa
mapambano hayo katika jamii.
Waziri wa katiba
na sheria Dkt.Augustine Mahiga amesema rushwa ni maradhi ambukizi na
isipokomeshwa inaiva hivyo yake imeendelea kusimamia sheria kuhusiana
na kuwabana wala rushwa hususan kuanzisha mahakama maalum ya kupambana
na Mafisadi.
Waziri wa Elimu
,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako amesema vijana hususan
Shuleni wanatakiwa kuwa chachu na kufanya mabadiliko katika mapambano
dhidi ya rushwa ambapo amesema wizara yake itashirikiana na TAKUKURU
pamoja na Skauti Tanzania katika kuwasimamia vijana katika mapambano
hayo.
No comments :
Post a Comment