Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya
Magharibi – Sospeter Magesse (kushoto), akimkabidhi tisheti 1800 Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu – Jumanne Sagini kwa ajili ya maadhimisho ya
Siku ya Wanawake Duniani.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Wakati Mkoa wa Simiyu ukiwa
mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Kitaifa Machi 8,
2020, Benki ya NMB imenogesha maadhimisho hayo kwa kutoa msaada wenye
thamani ya sh. Milioni 26.
Msaada huo ni pesa taslimu kiasi
cha sh. Milioni tano pamoja na tisheti zenye thamani ya Sh. Milioni 21,
ambapo umekabidhiwa na Meneje wa Beki hiyo Kanda ya Magharibi Sospeter
Magesse.
Akipokea msaada huo Katibu Tawala
wa Mkoa Jumanne Sagini, aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo walioutoa
ambao alieleza utasababisha maadhimisho hayo kupendeza.
Sagini alisema kuwa NMB imekuwa
benki pekee na mdau mkubwa wa maendeleo katika Mkoa wa Simiyu, kwani kwa
miaka miwili mfululuzo imekuwa ikidhamini maazimisho ya siku ya
wakulima kitaifa ambayo yamefanyika mkoani hapo.
Alisema kuwa Ofisi ya Mkoa
inamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, kwani kila wanapowasilisha
maombi ya msaada wowote kwake amekuwa hasiti kusaidia.
“ Tunajua NMB imeshiriki
mambo mengi kwenye Mkoa wetu ya maendeleo, kwenye Nanenane ambayo mwaka
huu inafanyikia hapa kwa mara ya tatu, NMB wamekuwa wakishiriki
kudhamini kila mwaka,” alisema Sagini.
Aliongeza kuwa, maandalizi yote yamekamilika na mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan.
Kaba ya kukabidhi msaada huo,
Meneja huyo wa Kanda wametoa tisheti 1800 ambazo zitavaliwa na washiriki
wote wa maazimisho hayo pamoja na pesa sh. Milioni tano kwa ajili ya
kusaidia kukamilisha maandalizi.
Magesse alisema kuwa benki hiyo
itaendelea kuwa mshirika mkuu na mkubwa wa maendeleo katika mkoa wa
Simiyu, huku akitumia nafasi hii kuwataka wanawake kuchangamkia fursa ya
mikopo midogo inayotolewa na benki hiyo
No comments :
Post a Comment