Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama
akiangalia ramani ya Safari za Wafanyabiashara ya watumwa iliyoko
katika jumba la makumbusho(Caravan Serai) lililoko Bagamoyo ambalo
lilitumiwa na wafanyabiashara hao kama sehemu ya kupumzika baada ya
kusafirisha watumwa kwa umbali mrefu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika,
baada ya kutembelea maeneo hayo kwa ajili ya kukagua maeneo
watakayotembelea mawaziri wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa
Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama,
akipokea maelezo kutoka kwa mwongoza watalii wa jumba la
makumbusho(Caravan Serai) lililoko Bagamoyo kwa ajili ya kukagua maeneo
watakayotembelea mawaziri wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa
Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC.
Moja ya picha ikionesha mtumwa
amebeba pembe za ndovu katika kituo walichokuwa wakipumzika katika moja
jumba la makumbusho(Caravan Serai) lililoko Bagamaoyo ambalo lilitumiwa
na wafanyabiashara hao kama sehemu ya kupumzika baada ya kusafirisha
watumwa kwa umbali mrefu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Ajira Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama
akimsikiliza mwongoza watalii alipokuwa akieleza kuhusu jumba la Ngome
Kongwe lililoko Bagamoyo ambalo lilitumiwa na wafanyabiashara ya utumwa
kama sehemu ya kupumzika kabla ya kupeleka watumwa katika soko dogo la
watumwa lililokuwa Bagamoyo, katika mwendelezo wa kukagua maeneo
watakayotembelea mawaziri wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa
Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Walemavu, Jenista Mhagama
akimsikiliza mwongoza watalii alipokuwa akieleza kuhusu bandari
iliyotumika kusafirisha watumwa kwenda Zanzibar iliyoko Bagamoyo ambalo
bandari hiyo ilitumiwa sana na wafanyabiashara ya utumwa kama Sehemu
kupeleka watumwa katika soko Kuu la Watumwa lilokuwa Zanzibar, baada ya
kutembelea maeneo hayo ikiwa ni moja ya maandalizi ya Mkutano wa
Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama
akimsikiliza mwongoza watalii alipokuwa akieleza kuhusu jumba la
makumbusho ya Kanisa Katoliki lililoko Bagamoyo ambalo linaelezea juhudi
za kukomesha biashara ya utumwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama,
akisoma moja ya kumbukumbu iliyoko kwenye jumba la makumbusho ya Kanisa
Katoliki lililoko Bagamoyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama akiwa na baadhi ya
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu
wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC, akisikiliza maelezo kuhusu nyumba
aliyokuwa akiishi mpigania uhuru wa Msumbiji, Hayati Samora Machael
iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani walipotembelea leo kukamilisha maandalizi
ya Mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania
Nyumba alimokuwa akiishi
mpigania uhuru wa Msumbiji, Hayati Samora Machael iliyoko Bagamoyo
Mkoani Pwani, mara baada ya kutembelewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Walemavu, Jenista
Mhagama akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri
na Wadau wa Utatu wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC utakaofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Tanzania.
Moja ya eneo kongwe la
makumbusho la Kaole lililoko Bagamoyo Mkoani Pwani kama linavyoonekana
kwenye picha mara baada ya kutembelewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista
Mhagama akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri
na Wadau wa Utatu wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC utakaofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama
akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri na
Wadau wa Utatu wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC wakimsikiliza mwongoza
watalii wa makumbusho ya Kaole, Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama akiwa na
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu
wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC wakiangalia maji ya kisima kilichopo
katika makumbusho ya Kaole, Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana, na Walemavu, Jenista Mhagama akionesha kaburi la
wapendanao kwa Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri na
Wadau wa Utatu wa Sekta ya Kazi na Ajira wa SADC katika makumbusho ya
mambo ya kale Kaole, Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi,Ajira Vijana, na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama akiwa na Wajumbe wa
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Sekta
ya Kazi na Ajira wa SADC wakipata maelezo kuhusu makaburi ya watoto
wadogo waliofariki yaliyoko katika makumbusho ya mambo ya kale Kaole
Bagamoyo Pwani, Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
No comments :
Post a Comment