Thursday, March 5, 2020

Vodacom Tanzania yadhamini Wiki ya Ubunifu 2020



Naibu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo UK AID, Natalie Smith akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation Week 2020) leo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa  COSTECH, Dkt. Amos Nungu (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation Week 2020) leo jijini Dar Es Salaam. Katika wiki hiyo ya ubunifu ambayo kauli mbiu yake ni “Buni kwa Tija” Kampuni ya Vodacom ni mdhamini mkuu wa maadhimisho hayo. Wengine toka kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkazi UNDP, Sergio Valdini, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Bi.Rosalynn Mworia, na Naibu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo UK AID, Natalie Smith.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Bi.Rosalynn Mworia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation Week 2020) leo jijini Dar Es Salaam. Katika wiki hiyo ya Ubunifu ambayo kauli mbiu yake ni “Buni kwa Tija” Kampuni ya Vodacom inatarajia kuonyesha bunifu zake mbalimbali katika sekta ya Kilimo, Elimu, Fedha na Afya. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa  COSTECH, Dkt. Amos Nungu, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo UK AID, Natalie Smith na Mkurugenzi Mkazi wa HDIF, Joseph Evarist.

No comments :

Post a Comment