Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kamati
ya kudumu ya bunge ya masuala ya Ukimwi imeusifia mkoa wa Arusha kwa
kushuka kwa kiwango Cha maambukizi ya ukimwi kutoka mwaka 2003 /4
ulikuwa ni asilimia 5.1 hadi asilimia 1.9 mwaka 2016/17.
Akiongea
na wanahabari Mara baada ya ziara yao ya siku mbili mkoani hapa
kutembelea Magereza na Hospital ya mkoa ya Mount Meru Mwenyekiti wa
kamati ya kudumu ya masuala ya Ukimwi Kifua kikuu na madawa ya kulevya
Oscar Mukasa alisema kuwa wamefurahishwa Sana na mkoa huo kwenye suala
hilo la kushuka kwa viwango vya maambukizi ya Ukimwi.
Alisema
kuwa mafanikio ya Kwanza kwenye hospital ya Mont Meru ni suala zima la
Usafi kwenye hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na shughuli za huduma za
utoaji dawa CTC wamejipanga vizuri na taarifa yao inaonyesha mafanikio
makubwa japo Kuna changamoto kidogo.
Alisema
kuwa changamoto kubwa ni taarifa ya wagonjwa kutoendelea na dawa nao
wameshauri watumie huduma ya kuwafuata majumbani kwani wamebaini kuwa
wengi wasioendelea na dawa ni wagonjwa wa nje ambao wanakaa mbali na
hospital hiyo hivyo kuwataka kusogeza huduma hizo kwenye vituo vya
karibu na wagonjwa hao.
“Utaona
mkoa huu umeweza kupunguza maambukizi ya Ugonjwa huu na inafanya vizuri
mfano ni hospitali ya mkoa ya Mount Meru ipo Safi hili ni kiashiria
kizuri Cha utoaji wa huduma bora Ila changamoto inatakiwa wasogeze
huduma kwa wagonjwa kwenye vituo vya Afya vyote ili kuweza kuwahudumia
kwa ukaribu zaidi” alisisitiza Mukasa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kinga wizara ya Afya Dkt.Leonard Subi alisema
kuwa uwasilishaji wa taarifa kwa watendaji wamelichukuwa huku Serikali
ikiwa na malengo ya kufikia tisini Tatu kwenye zile tisini Tatu.
Alisema
kuwa vituo vya kutibu Ugonjwa wa kifua kikuu ni 144 ambapo hapo awali
mwaka 2005 hospital ya kibongoto ilikuwa pekee ikitibu Ugonjwa huo hapa
nchini na hii ni mafanikio makubwa Sana ya Serikali ya awamu ya tano
chini ya Dkt.John Magufuli kuweza kujenga hospitali na vituo vya Afya
kila Kona ya nchi.
“Utaona
mafanikio makubwa tumeweza kuzifikia tisini Tatu kwa asilimia kubwa
mfano tisini ya Kwanza ni sawa na asilimia karibu 87 ambayo ni ya watu
wanaojua hali zao na wanatumia dawa huku tisini ya pili ikiwa ni
asilimia 85 na tisini ya Tatu ni asilimia 87 hadi 88 utaona jinsi
mafanikio yalivyo” alisema Dkt.Subi
Awali
mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa Mbulu Vijijini Fratey Massay alisema
kuwa mafanikio hayo yanaonyesha ushirikiano uliopo Kati ya viongozi na
watendaji hivyo suala hilo la kupunguza kwa maambukizi mapya linahitaji
ushirikiano huo utakaosaidia kuendelea kupunguza maambukizi na kutoa
huduma za Afua za Ukimwi.
No comments :
Post a Comment