Ujumbe kutoka Burundi wakiwa
kwenye majadiliano wakti walipotembelea chumba cha tiba ya mionzi ya 3D
kinachotumia mashine za Linac. Ugeni huo upo nchini ukijifunza katika
taasisi ya Saratani ya Ocean road
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road(ORCI) Dk. Julius Mwaiselage akizungumza uwepo wa
ugeni kutoka Burundi kuja kujifunza utendaji wa taaisisi juu ya kutibu
magonjwa ya Saratani
Moja ya mashine ys LINAC ambayoa inatibu magonjwa ya saratani kibingwa ikiwa katika muonekano tofautitofauti
Ujumbe huo wa kutoka Burundi wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya kutembelea vitengo ndani ya Taasisi hiyo ya Ocean Road.
Ujumbe kutoka Burundi wakiwa
kwenye majadiliano wakti walipotembelea chumba cha tiba ya mionzi ya 3D
kinachotumia mashine za Linac. Ugeni huo upo nchini ukijifunza katika
taasisi ya Saratani ya Ocean road
Daktari Bingwa wa magonjwa ya
Saratani wa ORCI, Dk. Nanzoke Mvungi akitoa maelezo kwa ugeni kutoka
Burundi ambao wapo hapa nchini kujifunza
……………………………………………
UJUMBE wa wataalam wa watu watano
wakiwemo Madaktari na maafisa kutoka Wizara ya Afya ya Burundi upo
nchini kwa ziara maalum ya siku tano kujifunza mambo mbalimbali ya
utendaji na uendeshaji unaofanywa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
(ORCI) ikiwemo namna inavyotoa huduma zake za matibabu kwa wagonjwa wa
Saratani kwa ubora Ukanda wa Afrika Mashariki.
Ugeni huo pia utapata nafasi ya
kujifunza kwa nadharia na vitendo ambapo watazunguka katika kujionea
jinsi huduma zinavyotolewa na namna wanavyoendesha matibabu ikiwemo
kutumia mitambo ya kisasa inayotumia miale ya mionzi mashine ya Linac
Accelerator ambayo inapatikana Tanzania pekee kwa Ukanda huu wa Afrika
Mashariki.
Awali akizungumza na waandishi wa
Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage amesema
wameupokea ujumbe huo kutoka Burundi ambapo utakuwa Nchini kwa siku
tano na kujifunza ili kupata uzoefu ambapo nao wakiwa mbioni kuanzisha
huduma kama hizo nchini mwao.
‘ORCI tuna ujumbe kutoka Burundi
umekuja hapa Tanzania, kuangalia na kujifunza maendeleo katika hutoaji
wa huduma za saratani hapa nchini.
Kama inavyofahamika ukanda huu wa
Afrika hususani Tanzania, ORCI imepiga hatua kubwa sana katika utoaji
wa huduma za saratani kwa wananchi wake hivyo Shirika la kimataifa la
nguvu za atomic – IAEA limeona ni busara sana kwa zile nchi ambazo
zinataka kuanzisha huduma zake za saratani, zifike Tanzania hapa kwetu
ili kujifunza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika kwa weredi na kwa
upana mkubwa sana.
‘Tumepata hii timu ya kutoka
Burundi ambao tutakuwa nao hapa kwa siku tano na kujaribu kuonyesha na
kuwaelezea tulivyofanya kwa kupitia uboreshaji wa huduma kutibu
saratani kwenye vituo, uboreshaji wa tiba ya kutibu kwenye Kanda, na
uboreshaji wa Ocean road kupitia kununua mashine mpya.
Pia uboreshaji wa tiba kemia,
upatikanaji wa dawa pamoja na mafunzo kwa watumishi wa Afya katika
utoaji wa huduma ya saratani.’ Alisema Dk. Mwaiselage.
Dk. Mwaiselage ameipongeza
Serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha taasisi hiyo kiasi kwa sasa
imekuwa kimbilio kwa nchi nyingi ambazo zinataka kuja kujifunza namna ya
tiba ya Saratani.
‘ORCI tunaipongeza na
tunashukuru kwa msaada mkubwa kutoka Serikali, na hasa serikali hii ya
awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kipindi hiki cha miaka minne
taasisi imekuwa mbele sana katika hutoaji wa huduma na nchi nyingi
imeona Tanzania tukipiga hatua kwenye kutibu saratani ikiwemo kununua
mashine hizi mionzi za kisasa za LINAC ambazo zinapatikana katika nchi
chache sana za Afrika huku zikipatikana nchi chache za Ulaya, India na
Marekani.’ Alisema Dk. Mwaiselage.
Dk. Mwaiselaga amesema
wamejitahidi katika upatikanaji wa dawa za saratani ambazo zinapatikana
kwa kiwango kikubwa sana na wagonjwa wanatibiwa vizuri.
‘Utaratibu wa Tanzania wa kununua
dawa ni mzuri sana tunatumia Bohari kuu ya Dawa ‘MSD’ ambapo Serikali
inatoa fedha zinaenda huko na MSD wananunua dawa kiwandani nah ii
inafanya upatikanaji wa dawa na tiba kuwa mzuri na wagonjwa wengi
ikiwemo nje wanafika hapa kupata hduuma hii ambapo pia tumeboresha
huduma zaidi. Lengo ni kuona watanzania wote wanapata huduma hapahapa
bila kwenda nje ya nje ya Nchi’ alieleza Dk. Mwaiselage.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya
Saratani Nchini Burundi, ambaye alionge kwa niaba ya ujumbe huo, Dk.
Jonas Nsegiyumva alieleza kuwa, Burundi inaendelea kuona namna ya
kuzuia ugonjwa huo wa saratani ikiwemo kuwapatia tiba wananchi wake
ambapo ujio wao hapa nchini utakuwa chachu ya kwa Taifa lao.
‘Tumeshukuru kuja hapa Taasisi ya
Ocean Road kujifunza dhidi matibabu ya Saratani, tumeona Madaktari ni
wengi tena ambao wanauwezo ambao wanaweza kutibu watu. Pia wana wagonjwa
wengi wakiwa wanatibiwa vizuri sana.
Kwa sasa hivi nchini kwetu ndio
tumeanzisha Taasisi yetu ijulikanayo kama Taasisi ya Saratani
Bujumbura na mwaka mmoja ama miwili tunaweza kusema ni idadi ya
wagonjwa wangapi wa saratani . Kwa Burundi saratani zinazosumbua kwa
sasa ni saratani za kike, saratani ya utumbo na zingine nyingi.’
Alisema Dk. Nsegiyumva.
Aidha, ORCI imeeleza kuwa kwa
sasa wanatarajia kuendelea kupokea ugeni mwingine kama huo kutoka nchi
mbalimbali zikiwemo za Liberia na Lethoto ambazo zitafika nchini
kujifunza juu ya utoaji na tia ya Saratani.
No comments :
Post a Comment