NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa
Aweso,akizungumza na washiriki wakati akifungua mkutano wa mrejesho wa
uhakiki na tathmini ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu
ya nne(PBR) inayotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya
Kimataifa ya Uingereza(DFID), uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki kutoka sehemu
mbalimbali wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maji, Jumaa
Aweso,wakati akifungua mkutano wa mrejesho wa uhakiki na tathmini ya
utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu ya nne(PBR)
inayotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya
Uingereza(DFID), uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof.
Kitila Mkumbo,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa
uhakiki na tathmini ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu
ya nne(PBR) inayotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya
Kimataifa ya Uingereza(DFID), uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya
Maji,Mhandisi Anthony Sanga,akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa mrejesho wa uhakiki na tathmini ya utekelezaji wa mpango wa
malipo kwa matokeo awamu ya nne(PBR) inayotekelezwa kwa ufadhili wa
Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza(DFID), uliofanyika jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Wakala wa Maji na
Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa), Mhandisi Clement Kivegalo,akitoa
tathmini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa uhakiki na
tathmini ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu ya
nne(PBR) inayotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa
ya Uingereza(DFID), uliofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Idara ya Maendeleo
ya Kimataifa ya Uingereza(DFID), Getrude Kihunrwa,akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa uhakiki na tathmini ya utekelezaji
wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu ya nne(PBR) inayotekelezwa kwa
ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza(DFID),
uliofanyika jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa
Aweso,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka sehemu mbalimbali
mara baada ya kufungua mkutano wa mrejesho wa uhakiki na tathmini ya
utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu ya nne(PBR)
inayotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya
Uingereza(DFID), uliofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa
Maji Jumaa Aweso amezitaka mamlaka za Maji kufanya uwiano ulio
sawa wa
Ulipaji wa gharama za maji kati ya Maeneo ya mjini na vijijini .
Kauli hiyo
ameitoa leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mrejesho wa
uhakiki na tathmini ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokeo awamu
ya nne(PBR) inayotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya
Kimataifa ya Uingereza(DFID).
“Ukiangalia
maji yanayotumika DSM,Maji yanayotumika Mwanza na Maeneo mengine mjini
kwa maana ,maeneo ya vijijini wananchi wanatumia maji kwa gharama kubwa
sana ,mfano Unit 1 ya Maji DSM inanunuliwa kwa Tsh.1800 lakini ukienda
vijijini unit 1 mwananchi ananunua mpaka Tsh.5,000 ,hili jambo si
sahihi na Unit 1 sawa nan doo hamsini ,hivyo mamlaka mnaohusika na
huduma ya usambazaji wa maji mnatakiwa mliangalie sana”.amesisitiza
Mhe.Aweso
“Nikuombe sana Mkurugenzi wa
Ruwasa jukumu letu ni kuhakikisha mwananchi wa mijini na vijijini
wanapata huduma nafuu, lazima tuangalie namna ya kumpa mwananchi unafuu,
vijijini wananunua maji kwa gharama kubwa,”amesema Mhe.Aweso
Aidha amesema
kuwa maeneo yaliyo kuwa na miradi ya maji kichefuchefu likiwemo eneo
la Mwakitolyo Mkoani Shinyanga sasa tayari serikali ilishachukua hatua
ya kumfukuza mkandarasi na kinachofanyika ni kuwatumia wataalam wa ndani
ili huduma ya maji ipatikane kwa wananchi.
Katibu Mkuu
wizara ya Maji,Prof.Kitila Mkumbo amesema Serikali pamoja na Wadau
wameshatekeleza miradi ya Maji 1423 tangu mwaka 2015 hadi sasa ,kati ya
hiyo miradi 792 ilishakamilika mpaka kufikia mwezi Disemba Mwaka
jana na serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 631.
Kwa upande wake Naye, Naibu Katibu
Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga amesema kuwa kuna kero
kubwa ya maji vijijini hivyo bila kuwa na takwimu kwenye utendaji kazi
watakwama.
Awali, Mkurugenzi
wa Ruwasa, Mhandisi Clement Kivegalo, amesema kuwa katika awamu hiyo ya
nne ya mpango huo ambayo inatekelezwa na Ruwasa, Halmashauri 181
zilifuzu ambapo Sh.Bilioni 63.46 zimetolewa.
“Hii ni sawa na
ongezeko la takribani asilimia 110 ni zaidi ya mara mbili ya kiasi
kilichotolewa katika awamu ya tatu, hata hivyo bado kuna maeneo ambayo
tathmini inaonesha kuwa baadhi ya halmashauri hazikufanya vizuri katika
vigezo vinavyotajwa,”amesema Sanga
Naye, Mwakilishi wa
Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza(DFID), Getrude Kihunrwa ,
amesema kwasasa hali ya utekelezaji wa miradi unakwenda vizuri kwani
hapo mwanzo walitamani hata kuachana na kutekeleza mradi huo lakini kwa
Sasa hali ni safi na wataendelea kushirikiana na serikali katika
kutekeleza miradi hiyo.
“Hali ya utekelezaji wa
Mradi huu kwa Sasa unaridhisha kwa mwanzo hali haikuwa shwari, kabisa,
lakini kwa Sasa mambo yanakwenda sawa, mfano ni Wilaya ya Gairo ambayo
ilikuwa ikifanya vibaya, lakini leo ni moja ya Wilaya zilizopokea zawadi
kwa kufanya vizuri” amesema Bi Getrude.
No comments :
Post a Comment