Moja ya Daraja lilisombwa na maji Manispaa ya Morogoro
………………………………..
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
Mvua zinazonyesha mkoani Morogoro
zimeendelea kuleta madhara, ambapo baadhi ya
Madaraja yamesombwa na maji
na kufanya baadhi ya mitaa kutofikika, Mito mikubwa kufurika ukiwemo
Mto Morogoro na Mto Mkundi iliyokatiza katikati ya Mji hivyo maji
kutiririka kuelekea katika makazi ya watu.
Hata hivyo Wakazi waliopembezoni
mwa mito hii mikubwa ukiwemo Mto Morogoro na Mto Mkundi wanasema, pamoja
na hali hii kusababishwa na Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha, Dalili
za Mmomonyoko zilionekana wazi hata kabla ya msimu wa Mvua.
Akizungumza na waandishi wa habari
Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Mnene
James wamesema hatua za uchunguzi zinaendelea, mpango ni kuchukua hatua
za haraka kurejesha mawasiliano katika maeneo hatarishi.
Pamoja na uharibifu wa
Miundombinu, imesha ripotiwa baadhi ya watu kupoteza maisha msisitizo ni
wananchi kuchukua tahadhari hasa waishio mabondeni na wale wa
pembezoni mwa mito Mikubwa.
No comments :
Post a Comment