Meneja wa mafunzo wa Wakala ya
Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Brown Hasunga,akitoa taarifa ya
awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya menejimenti ya TMA yaliyofanyika
leo jijini Dodoma (katikati) Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk Leonard
Chamuriho na kushoto ni Mkurugenzi wa TMA Dk Agnes Kijazi
Mkurugenzi wa TMA Dk Agnes
Kijazi,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya TMA yenye lengo la
udhibiti na ukusanyaji wa mapato ya huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo
yaliyofanyika leo jijini Dodoma kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi
Dk Leonard Chamuriho ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk
Leonard Chamuriho,akizungumza na washiriki wakati akifungua mafunzo ya
TMA yenye lengo la udhibiti na ukusanyaji wa mapato ya huduma
zinazotolewa na mamlaka hiyo yaliyofanyika leo jijini Dodoma kushoto
kwake ni Mkurugenzi wa TMA Dk Agnes Kijazi.
Sehemu ya washiriki wakifatilia
hotuba ya Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho,wakati wa
ufunguzi mafunzo ya TMA yenye lengo la udhibiti na ukusanyaji wa
mapato ya huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo yaliyofanyika leo jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk
Leonard Chamuriho akiwa kwenye picha ya pamoja na na washiriki mara
baada ya kufungua mafunzo ya TMA yenye lengo la udhibiti na ukusanyaji
wa mapato ya huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo yaliyofanyika leo
jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) imepewa ruhusa ya kuwatoza fedha wahitaji
takwimu za hali ya hewa
za usanifu miradi mbalimbali ikiwemo wa majengo ili kufanya kazi ya
usanifu.
Kauli hiyo imetolewa leo
jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho
wakati akifungua mafunzo ya menejimenti ya TMA yenye lengo la udhibiti
na ukusanyaji wa mapato ya huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo.
Dk.Chamuriho amesema TMA imelega
kukusanya mapato katika huduma inazozitoa ni vyema wasanifu hao
wakaweza kutozwa fedha hizo ili kurudisha gharama zilizotumika wakati
wa kuandaa takwimu hizo.
“Mkumbuke kuwa hapa mnaongea na
Mhandisi wa ujenzi hivyo kwenye kazi zetu za usanifu huwa tunakuja kwenu
kuhitaji takwimu kutoka hali ya hewa mfano kwa sasa tunasanifu majengo
marefu tunahitaji kujua nguvu ya upepo kwa kila urefu unapokwenda hivyo
sio dhambi na ninyi mkitoza hizo takwimu kwani zinakwenda kutumika
kibiashara”amesema Dk.Chamuriho
Aidha Dk.Chamuriho amesema kuwa
wanaosanifu muindombinu ya ujenzi kama vile madaraja wanataka kujua
mtiririko na wingi wa maji ili waweze kusanifu madaraja hayo kama
yanaweza kuhimili nguvu za asili,takwimu hizo zinapatikana kwenu.
Hata hivyo ameongeza kuwa ubora
wa huduma za hali ya hewa umezidi kuongezeka na kuonekana kwa jamii kwa
kiwango kikubwa, hivyo jitihada hizo zitumike pia katika ukusanyaji wa
mapato na udhibiti wa huduma za hali ya hewa nchini.
Amesema kwa sasa serikali imeanza
kufunga rada mkoa wa Mtwara na wanataraji kuanza kufunga nyingine
katika mikoa ya Mbeya ya Kigoma, kwa lengo la kutimiza makubaliano ya
kimataifa ambayo serikali iliridhia kubadilishana taarifa kwa njia ya
mtandao wa dunia (Global Telecommunication System).
Awali Mkurugenzi wa TMA Dk Agnes
Kijazi, amesema kuwa ili kuweka msingi imara kwa TMF mafunzo hayo
yatawafanya kuwa na uwezo wa kutoa huduma bora zaidi kwa kukidhi
mahitaji ya wadau nchini.
Dk.Kijazi amesema kuwa katika
mafunzo hayo wanafunzi watahusika kufanya mazoezi mbalimbali na
majadiliano kwa lengo la kuinjengea menejimenti ya TMA uwezo katika
maeneo ya udhibiti na ukusanyaji wa mapato katika huduma wanazotoa.
Amesema kuwa viwango vya usahihi
wa utabori wa hali ya hewa umezidi kuimarika kwa mikaa 10 hadi kufikia
zaidi ya asilimia 80 huku kiwango cha chini kilichowekwa na shirika la
hali ya hewa duniani cha asilimia 70.
Kwa Upande wake Meneja wa mafunzo
wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Brown Hasunga amesema
kuwa wameamua kutoa mafunzo hayo ili kuongeza uelewa kwa menejimenti ya
mamlaka hiyo baada ya TMA kubadilika kutoka wakala hadi kuwa mamlaka.
No comments :
Post a Comment