*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Makamu mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Bara, Mhe.Philip Mangula imegundulika amewekewa sumu baada
ya uchunguzi kufanyika na kubaini hivyo ijapokuwa
bado haijajulikana
aliwekewa kwa njia ipi.
Ameyasema hayo leo, Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa katika mkutano na
wanahabari Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano huo,
Kamanda Mambosasa amesema kuwa taarifa hizo walizipata Februari 28 mwaka
huu baada ya mzee huyo kudondoka ghafla katika ofisi ndogo ya chama
Lumumba Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kikao cha kamati kuu
ya halmashauri kuu ya Taifa.
“Katika taarifa hiyo tulielezwa
kwamba, Mzee Mangula alipelekwa Muhimbili na kulazwa ICU, Jeshi la
polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
limebaini kwamba ndani ya mwili wa Mzee Mangula ulipatikana na sumu, kwa
yeyote atakayebainika kupanga, awe ndani ya CCM, mwanafamilia ama
Serikalini hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ” amesema Kamanda
Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa amesema
kuwa upelelezi kuhusu namna ambavyo sumu hiyo iliingia mwilini bado
unaendelea, na Jeshi hilo halitasta kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote
atakayebainika aliyehusika na uhalifu huo.
No comments :
Post a Comment