**************************
Na Magreth Mbinga
Serikali imewataka watu hasa
waishio vijijini kupitia changamoto walizonazo kuibua ubunifu ili
kukabiliana na changamoto za kiuchumi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri
wa elimu sayansi na teknolojia William Olenasha katika
ufunguzi wa wiki
ya ubunifu iliyofanyika katika Kijiji cha makumbusho jijini Dar es
salaam.
“Nimezindua wiki ya ubunifu ambayo
inakutanisha wadau na wabunifu mbalimbali kwaajili ya kutambulisha
bidhaa zao ambazo wanabuni”alisema Olenasha.
Pia Olenasha amesema kama Tanzania
inataka kukuza uchumi kwa kutegemea viwanda lazima iwe na wabunifu ndio
maana wameanzisha mashindano ya wabunifu Taifa yatakayo fanyika mjini
Dodoma.
Vilevile Mkurugenzi wa NHIF Joseph
Evalisti amesema wao ndio waandaaji wa wiki ya ubunifu wameandaa
tamasha hilo ili kuwakutanisha wabunifu na kuwafanya watambulike na watu
mbalimbali.
“Tulianza na watu sita tulijikita
zaidi hapa Dar es salaam kwa sasa tuna wabunifu wengi na tunataka twende
nje ya mkoa huu wiki ijayo tunazindua wiki ya ubunifu Dodoma” alisema
Joseph.
Hatahivyo mkurugenzi wa sayansi na teknolojia Dk Amosi Nungu
amewataka vijana wajitokeze kwa wingi ili serikali iwasaidie kukuza
ubunifu wao mpaka sasa wamewasaidia vijana sitini katika kuendeleza
ubunifu wao katika nyanja mbalimbali.
No comments :
Post a Comment