Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe,(Mwenye tai) na Kiongozi
wa ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani, Kutoka Wizara ya
Afya nchini Sudani, Huda Kambal (mwenye Ushungi), wakifuatilia kikao cha
kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa
vyakula nchini, maafisa hao wamekuja kujifunz hapa nchini kuhusu masuala
hayo, Machi 2020 Jijini Dodoma
Baadhi ya maafisa waandamizi
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na maafisa waandamizi kutoka nchini
Sudani, wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa
masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini, yanayoratibiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, Machi 2020 Jijini Dodoma.
Baadhi ya maafisa waandamizi
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na maafisa waandamizi kutoka nchini
Sudani, wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa
masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini, yanayoratibiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, Machi 2020 Jijini Dodoma.
Baadhi ya maafisa waandamizi
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu
kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini,
yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Machi 2020 Jijini Dodoma.
Baadhi ya maafisa waandamizi
kutoka nchini Sudani, wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu
uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini,yanayoratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu, Machi 2020 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa
Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul
Sangawe, akiongoza kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini na Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani waliokuja hapa nchini kupata uzoefu huo, Machi 2020 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa
Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul
Sangawe (Mwenye tai), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani mara baada ya kumaliza kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini, Machi 2020 Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………..
Na. OWM, DODOMA
Ujumbe wa maafisa
waandamizi wa serikali kutoka nchini Sudani umekuja hapa nchini
kujifunza masuala ya Uratibu wa Vuguvugu la Lishe na urutubishaji wa
Vyakula. Ofisi ya
Waziri Mkuu imekuwa ikiratibu masuala ya lishe nchini
kutokana na mamlaka iliyonayo kikatiba ya kuratibu shughuli zote za
Serikali pamoja na masuala mtambuka. Uratibu huo unafanywa kupitia
Kamati ya kitaifa ya Lishe chini ya Uongozi wa Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko.
Tanzania kupitia
Ofisi hiyo imefanikiwa kuandaa Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya
Lishe ambao hutoa mwongozo wa utekelezaji wa masuala ya Lishe nchini,
ikiwemo kupambana na upungufu wa ukosefu wa virutubishi kwa kuongeza
virutubishi hivyo kwenye vyakula, pamoja na uanzishwaji wa majukwaa
mengine ya lishe katika ngazi ya kitaifa hadi ngazi ya mkoa na wilaya
likiwemo jukwaa la sekta binafsi linalojikita sana kwenye masuala ya
urutubishaji wa vyakula.
Akiongea mara
baada ya kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Urutubishaji
wa vyakula, mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli
za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe, ambaye pia ni Mratibu
wa Vuguvugu la lishe nchini, amefafanua kuwa Tanzania ilikuwa
miongoni mwa nchi za awali duniani kujiunga na Vuguvugu la Lishe, ambalo
linahimiza ushiriki wa sekta zingine na wadau wa lishe kupambana na
utapiamlo wa watoto wa chini ya miaka mitano hasa aina ya udumavu.
“Kutokana na
utekelezaji mzuri wa Vuguvugu la Lishe tumefanikiwa kuwa na mtandao
mzuri wa Lishe wa kisekta kwa sekta binafsi, lakini pia utashi wa
kisiasa umeongezeka hapa nchini ambapo tayari takribani wabunge 55
wamejitanabaisha kujihusisha na masuala ya lishe. Masuala ya lishe
tayari yameingizwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa
miaka mitano (2016-2021) na Mwongozo wa Mpango na Bajeti ambao umesaidia
masuala ya lishe kuingizwa kwenye mipango ya kisekta ya nchi ”
amesisitiza Sangawe.
Aidha, Sangawe
amebainisha kuwa tayari Tanzania imefanikiwa kuwa na Kanuni za
Urutubishaji wa Vyakula za mwaka 2011, ambapo kanuni hizo zinavihusu
viwanda vikubwa vya uzalishaji wa vyakula hususan unga wa ngano na
mafuta ya kupikia.
Amesisitiza kuwa
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli,
imeendelea kulipa kipaumbele suala la lishe kwa kutoa muongozo kwa
Halmashauri zote nchini kutenga fedha za lishe kwa kila mtoto, ambapo
awali ilikuwa Shilingi 550/=, kwa kila mtoto na kwa sasa ni shilingi
1,000/= kwa kila mtoto.
“Kwa sasa
serikali imefanikiwa kuajiri wataalamu wa masuala ya lishe katika ngazi
ya Wizara na Halmashauri ambapo kwa sasa 57% ya Halmashauri 185 zote
nchini zimeajiri wataalamu wa masuala ya lishe huku Halmashauri
zilizobaki zina maafisa viungo tu wa masuala ya lishe ” Amesisitiza
Sangwe.
Amebainisha kuwa
serikali imeamua suala la lishe kuwa agenda ya Kitaifa ambapo kwa sasa
imeandaa makubaliano maalum (mikataba ya lishe) kwenye ngazi za serikali
za mitaa ambayo ni kati ya ngazi hizo na Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), lengo ni kuongeza uwajibikaji
kwenye masuala ya lishe.
Kwa upande wake,
Kiongozi wa ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani, Kutoka
Wizara ya Afya nchini Sudani, Huda Kambal, amefafanua kuwa wamechagua
kuja Tanzania kujifunza uratibu wa kisekta wa masuala ya lishe na
Urutubishaji wa vyakula hususani kwenye unga wa ngano na mafuta ya
kupikia.
“Sisi katika nchi
ya Sudani hatuna huu Uratibu wa kisekta katika masuala ya lishe na
Urutubishaji wa vyakula. Lengo la kuja hapa ni kujifunza na kutaka
kupata uzoefu wa namna ya kuratibu na kutekeleza shughuli za
Urutubishaji wa Vyakula hasa kwa wazalishaji wakubwa wa vyakula ili
twende tukaboreshe nchini kwetu shughuli hizo” Amesisitiza Kambal
Amebainisha kuwa
katika kuhakikisha wanafanikiwa kwenye kuanzisha Utaratibu huo
wanatarajia kujifunza na kupata uzoefu katika maeneo ya Udhibiti na
Usimamizi wa vyakula vilivyorutubishwa, ushiriki wa sekta binafsi kwenye
masuala ya lishe, ufuatiliaji wa mara kwa mara na mawasiliano kwa umma
juu ya masuala ya lishe.
Kikao hicho
kilihudhuriwa na maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu
wa Shughuli za serikali, Taasisi ya Lishe Tanzania, Shirika la Viwango
Tanzania pamoja na maafisa waaandamizi kutoka nchini Sudani ambao
wametoka Wizara ya Afya, Shirika la Chakula Duniani, Shirika la Afya
Duniani, Mamlaka ya Viwango na Ubora Sudani, Mamlaka ya utafiti na
Viwanda, Wizara ya Viwanda na Shirika la Biashara Sudani
Mnamo mwaka 2012
Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi za kwanza Duniani kujiunga kwenye
Vuguvugu la Lishe Duniani, ambapo mnamo mwaka 2011 aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kipindi hicho , Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kwanza kuingia kwenye
kikundi cha viongozi wa Vuguvugu la Lishe Duniani. Kuanzia Kipindi hicho
Agenda ya kitaifa ya masuala ya lishe ilianza kuratibiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu kama Ofisi yenye dhamana ya kuratibu shuguli za Serikali kwa
mujibu wa sheria.
No comments :
Post a Comment