Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akijadiliana jambo
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu
wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Marawakati
Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akifafanua jambo
kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Mara wakati
Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima
akielezea jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi William Lukuvi wakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
iliyopo mkoani Mara.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa
wa Mara Adam Malima wakikagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu Musoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha
shillingi Billioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali ya
Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa kwa miaka 40 bila
kumalizika.
Haya yamebainika
wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi katika hospitali hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.
Akizungumza mara
baada ya kutembelea Hospitali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali hiyo itakuwa
masaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara hasa kwa huduma za matibabu
ya kibingwa.
“Kutakuwa hakuna
haja ya kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kupata matibabu ya kibingwa
kwani tunataka huduma za kibingwa zitolewe hapa hapa”alisema
Kwa upande wake
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema
kuwa Shirika la Nyumba na Chuo Kikuu cha Ardhi kimepewa kazi ya
kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo hivyo ameagiza kazi kufanyika usiku
na mchana ili limalizike kwa muda uliopangwa.
“Tumekubaliana
tarehe 17 mwezi huu wa tatu wawe wamekamilisha Wing C ili huduma za Mama
na mtoto zinanze kutolewa kwa muda husika” alisema
Kwa upande wake
Mkuu Mkoa wa Mara Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya
kumalizia hospitali hiyo iliyokwama kwa muda wa miaka 40 mpaka sasa.
“Hospitali hii imechukua awamu tano za marais kumalizika na tunamshukuru Rais kwa kuchukulia kipaumbele katika hili” alisema
No comments :
Post a Comment