Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani
akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Machi 6, 2020. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU,
Kassim Majaliwa amewataka wananchi washirikiane na Serikali katika
kuwafichua wafanyabiashara wa magendo wanaoingiza bidhaa kwa kupitia
bandari bubu.
Pia ameiagiza
Idara ya Uvuvi wilaya ya Pangani ihakikishe inadhibiti uvuvi haramu wa
kutumia mabomu na nyavu zisizo stahili kwa kuwa unahatarisha mazalia ya
samaki.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 6, 2020) wakati akizungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Bomani,
wilayani Pangani.
Amesema uwepo
wa bandari bubu katika wilaya hiyo unasababisha kuingizwa kwa bidhaa
ambazo viwango vyake havijathibitishwa na mamlaka husika hivyo
kuhatarisha afya za watumiaji.
“Wananchi
shirikianeni na Serikali katika kuwataja wanaoingiza bidhaa kupitia
bandari bubu kwani licha ya bidhaa hizo kutokuwa na uhakika wa ubora,
pia hata wakwepakodi nao wanapitia huko.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu malalamiko ya wafanyakazi wa mkonge
ambapo amesema atamuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aende kushughulikia
suala hilo.
Kwa upande
wake, Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameishukuru
Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya
elimu, maji na umeme kwani kati ya vijiji 33 vya jimbo hilo vitatu tu
ndio havina umeme.
Pia mbunge
huyo ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali iharakishe utekelezaji wa
mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani yenye urefu wa kilometa 50
pamoja na ulipaji fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha mradi huo.
Awali, Waziri
Mkuu alizindua mradi wa ujenzi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani kwa
upande wa kaskazini wenye urefu wa mita 950 uliogharimu sh. Bilioni 2.9.
Pia alizindua kituo cha polisi cha wilaya ya Pangani pamoja.
No comments :
Post a Comment