BENKI ya NMB imekabidhi
misaada mbalimbali ya vifaa tiba na vifaa vya elimu katika Mikoa ya Dar
es Salaam na Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kurejesha kwa
jamii asilimia moja ya faida yao kupitia Programu ya Uwajibikaji kwa
Jamii (CSR).
Jijini Dar es Salaam, NMB imetoa
msaada yenye thamani ya Sh. Mil. 15 kwa Shule ya Sekondari Tambaza,
iliyopo Upanga na Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni wilayani Ilala jijini
Dar es Salaam, wakati Mkoani Kilimanjaro imekabidhi vifaa tiba kwa
Hospitali ya Wilaya ya Hai.
Tambaza Sekondari, imepokea
msaada wa vitanda 80 vya kulalia wasichana wa shule hiyo vyenye thamani
ya Sh. Mil. 10, vilivyokabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es
Salaam, Badru Idd na kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa
tiba katika Kituo cha Afya Pugu Kajiungeni, NMB ilikabidhi msaada huo
wenye thamani ya Sh. Mil. 5 kupitia kwa Meneja Mwandamizi wa NMB Kitengo
cha Biashara za Serikali, Adelard Mangombo, na kupokelewa na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala (DC), Sofia Mjema.
Mkoani Kilimanjaro, NMB kupitia
Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, alikabdhi msaada wa vitanda
vitano vya kulalia, viwili vya kujifungulia akina mama, mashuka 25,
magodoro 5, pamoja na hundi ya Sh. Milioni 16 kwa ajili ya wakulima wa
zao la vanilla Mkoani humo
Mkuu Wa Wilaya Mshikizi Agnes
Hokororo (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vinavyo tumika
wakati akina mama wakifujingua kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya
Kaskazini – Aikansia Muro.
Meneja Mwandamizi wa NMB
Kitengo cha Biashara za Serikali – Adelard Mang’ombo akimkabidhi msaada
wa vifaa vya afya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema ambavyo ni
vitanda vitano pamoja na mashuka katika Kituo cha Afya Pungu Kajungeni
vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 5.
NMB Karibu Yako
No comments :
Post a Comment